Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Shambulio la kemikali nchini Syria: Wachunguzi waruhusiwa kuzuru Douma


Wakaazi wakitembea karibu na eneo lililodaiwa kushambuliwa na kemikali Douma siku ya Jumapili wiki moja baada ya shambulio

Wachunguzi wa silaha za kemikali nchini Syria wataruhusiwa kuzuru katika eneo linalodaiwa kushambuliwa na silaha za sumu siku ya Jumatano, kulingana na uUrusi.


Kundi hilo la kimataifa limekuwa nchini humo tangu siku ya Jumamosi lakini halijaruhusiwa kuingia Douma.


Shambulio hilo la siku ya Aprili 7 lilivutia shambulio dhidi ya serikali ya Syria lililotekelezwa kwa pamoja na Marekani, Uingereza na Ufaransa wiki moja baadaye.


Syria na mshirika wake Urusi wamekana shambulio lolote la kemikali huku Urusi ikitaja madai hayo kama 'yaliopangwa'.


Mapema siku ya Jumanne , chombo cha habari cha Syria kilisema kuwa ulinzi wa angani wa taifa hilo ulikabiliana na shambulio la makombora juu ya nga ya magharibi mwa mji wa Homs.


Makombora hayo yalilenga kambi za wanahewa wa Shayrat lakini haikusema ni nani aliyetekeleza mashambulio hayo.


Image captionWaathiriwa wa shambulio nchini Syria

Ripoti nyengine kutoka kwa wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran-Hezbollah ilisema kuwa mtambo wa ulinzi wa angani ulitungua makombora matatu yaliolenga kambi ya wanahewa ya Dumair, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Damascus.


Msemaji wa Pentangon aliambia Reuters : Hakuna shughuli za kijeshi za Marekani katika eneo hilo wakati huo.


Ni nini kinachoendelea nchini Syria?


Mapema siku ya Jumamosi saa za Syria, Marekani, Uingereza na Ufaransa zilitekeleza mashambulio ya pamoja katika maeneo tofauti nchini Syria.


Operesheni hiyo ilikuwa ikijibu shambulio la silaha za kemikali iliotekelezwa na serikali ya Syria na kulenga raia na kuwaua makumi ya watu.


Wachunguzi kutoka shirika la kuzuia utumizi wa silaha za kemikali OPCW wako katika mji mkuu wa Damascus , lakini wamekuwa wakisubiri kuanza uchunguzi.


Wakati watakapowasili katika eneo hilo siku ya Jumanne, itakuwa siku 11 tangu shambulio hilo.


Wanatarajiwa kuchukua mchanga na sampuli kusaidia kutambua kemikalizilizotumika katika shambulio hilo.


Image captionWaziri wa maswala ya kigeni nchini Syria Sergei Lavrov

Mjumbe wa Marekani katika shirika la OPCW hatahivyo ameonyesha wasiwasi wake kwamba Urusi ilitembelea eneo hilo na huenda iliharibu ushahidi ili kuzuia uchunguzi.


Lakini katika mahojiano na BBC, waziri wa maswala ya kigeni nchini humo Sergei Lavrov alisema: Nawahakikishia kuwa Urusi haijaharibu ushahidi wowote katika eneo hilo.


Alisema kuwa ushahidi uliodaiwa na Marekani , Uingereza na Ufaransa ulitokana na habari za vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na kwamba ushahidi kama huo ni kitu kilichapangwa.


Bwana Lavrov na wengine pia wamekosoa mataifa hayo matatu kwa kutekeleza mashambulio hayo kabla ya kundi la wachunguzi wa OPCW kufanya uchunguzi wao.


Ni nini kinachodaiwa kufanyika katika shambulio la Douma?


Wakati shambulio hilo lilipodaiwa kufanyika tarehe 7 Aprili, Douma, katika eneo la mashariki mwa Ghouta, lilikuwa eneo linalodhibitiwa na waasi karibu na mji mkuu wa Damascus baada ya mwezi mmoja wa mashambulio.


Kwa sasa mji huo uko chini ya udhibiti wa majeshi ya Syria na Urusi.


Mabomu mawili yaliokuwa na kemikali yalidaiwa kuangushwa saa kadhaa tofauti katika mji huo.


Duru za kimatibabu nchini Syria zinasema kuwa miili kadhaa ilipatikana ikitoa mapovu mdomoni mbali na kuwa na ngozi iliokosa rangi na macho yaliochomeka.


Duru za Marekani zinasema kuwa zilipima sampuli za mikojo na damu kutoka kwa waathiriwa na kufanikiwa kupata kemikali ya khlorine na gesi ya neva


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...