Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mashambulizi dhidi ya Syria hayakuwa halali-Ripoti ya Bunge la Ujerumani

Ripoti ya wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani imesema mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Syria mapema mwezi Aprili yalikiuka sheria ya kimataifa.



Ripoti ya wataalamu wa sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani, imesema mashambulizi yaliyofanywa na nchi tatu za Magharibi hayakuwa halali kisheria. Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliishambulia Syria kwa makombora tarehe 14 Aprili, kwa madai kwamba zilikuwa zikiiadhibu serikali ya Rais Bashar al-Assad, ziliyemshutumu kutumia gesi ya sumu kuwashambulia raia katika mji wa Douma.


''Matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya nchi huru, kama hatua dhidi ya ukiukaji wa sheria na kanuni za kimataifa unaodaiwa kufanywa na nchi inayoshambuliwa, ni uvunjaji a sheria ya kimataifa inayozuia matumizi ya ghasia,'' imesema ripoti hiyo ya wataalamu wa kisheria wa Bunge la Ujerumani, Bundestag. Ripoti hiyo iliombwa na chama cha mrengo wa kushoto (Die-Linke) cha Ujerumani.

Azimio la Umoja wa Mataifa liko wazi

Wataalamu hao wa bunge walilinukuu azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la mwaka 1970, ambalo linatilia mkazo haja ya nchi, katika kuendeleza mahusiano mema ya kimataifa, kujizuia kutumia nguvu za kijeshi, za kisiasa, za kiuchumi au njia nyingine zozote za kushinikiza, dhidi ya uhuru wa nchi nyingine kisiasa, au kuingilia katika himaya yake ya kieneo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, alipigia debe mashambulizi dhidi ya Syria

Hali kadhalika, Umoja wa Mataifa unapinga ulipaji kisasi wa kutumia nguvu za kijishi, kwa hoja kwamba hauambatani na malengo na maadili ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa.

Aidha, ripoti hiyo ya wataalamu hao wa Bunge la Ujerumani, wamesema sababu zilizotolewa na Uingereza kama msingi wa kujiunga na Ufaransa na Marekani katika kuishambulia Syria, hazina mashiko. Mashambulizi hayo hayakupata ridhaa ya Umoja wa Mataifa.

Serikali mjini London ilidai kwamba inakubalika kisheria  kufanya mashambulizi ya kijeshi ili kuepusha mateso dhidi ya raia. Hata hivyo, wataalamu hao wa Ujerumani walisema yapi maswali yasio na majibu, juu ya iwapo mashambulizi ya nchi hizo tatu za Magharibi yatazuia madhila mengine kwa raia wa Syria.

Msimamo wa Ujerumani

Mwanzoni mwa mwezi huu wa Aprili, picha zilijitokeza katika vyombo vya habari, zikionyesha watu wanaopata shida kupumua, huku wakitokwa na mapovu mdomoni. Nchi za Magharibi ziliishutu serikali ya Rais Bashar al-Assad kufanya mashambulizi ya gesi ya sumu dhidi ya watu hao, madai ambayo Syria na washirika wake, Urusi na Iran waliyakanusha kwa nguvu.

Picha za watoto wanaoteseka kwa kile kinachodhaniwa kuwa shambulizi la gesi ya sumu kiliishitua dunia

Ingawa Ujerumani haikushiriki katika mashambulizi ya Aprili 14, Kansela Angela Merkel alisema mashambulizi hayo yalikuwa halali, na kwamba yalihitajika.

Wabunge wa chama cha Die-Linke, Heike HƤnsel na Alexander Neu wamesema ripoti hii ya wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa wa Bunge la Ujerumani ni pigo kwa serikali ya Kansela Merkel, naye msemaji wa Chama cha Kijani kuhusu masuala ya kimataifa, Omid Nouripour, ameitaka serikali ya Berlin kukiri hadharani kwamba ilisaidia ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Lakini Roderich Kiesewetter, msemaji wa muungano wa vyama vya kihafidhina unaoongozwa na Kansela Angela Merkel ametetea msimamo wa serikali, akisema ulikuwa wa busara, kwa sababu wakati mwingine inakuwa sahihi kutilia maanani hali halisi kisiasa, katika kuzuia ukiukaji wa sheria za kimataifa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...