Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ITALIA

Papa Francis amelazwa katika hospitali ya Gemelli kutokana na matatizo ya kupumua.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis (86), amelazwa katika hospitali ya Gemelli kutokana na matatizo ya kupumua. Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema kuwa katika siku za karibuni Kiongozi huyo amekuwa akilalamika kuhusu shida hiyo. Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki imeeleza matokeo ya vipimo kuwa ni tatizo kwenye mfumo wa upumuaji. Aidha Vatican imesisitiza kuwa Papa Francis hana Uviko19. Awali Vatican ilieleza kuwa Kiongozi huyo alipelekwa hospital ili kufanyiwa ukaguzi ambao ulishapangwa. Hata hivyo vyombo vya habari vya Italia vilihoji suala hilo kwani mahojiano ya televisheni aliyotakiwa kufanya Papa jioni ya leo yalifutwa dakika za mwisho.

Basi la shule latekwa na kuteketezwa Italia

Basi la shule nchini Italia likiwa limeteketea kabisa Basi lililokuwa limebeba watoto wa shule wapatao 51 lilitekwa na dereva wake na kisha kutiwa moto karibu na Milan nchini Italia. Watoto hao wa shule, baadhi yao walifungwa kamba, waliokolewa baada ya kuvunjwa vioo vywa basi hilo upande wa nyuma na hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa vibaya.Watu kumi na wanne waliathiriwa na moshi uliotokana na kuteketea kwa basi hilo. Dereva wa basi hilo alikuwa na umri wa miaka arobaini na saba mwenye uraia wa nchini Italia ingawa ana asili ya kutoka nchini Senegal, inaarifiwa kwamba ametiwa nguvuni. Dereva huyo alisikika akitamba, akiwaambia waliokuwemo katika basi hilo kwamba hakuna hata mtu mmoja atakaye nusurika.Ulikuwa ni muujiza, vinginevyo yangekuwa ni mauaji ya halaiki, alinukuliwa akisema hayo mwendesha mashtaa mkuu wa mjini Milan, Francesco Greco. Mwalimu mmoja wapo alikuwa ndani ya basi wakati tukio hilo likitekelezwa, alimuelezea mtuhumiwa huyo kuwa alikuwa na silika ya hasira mar...

KUTANA NA TIMU IYOFUNGWA GOLI 20 JUMAPILI HII

Klabu ya Pro Piacenza yalazwa 20-0 katika mechi ya ligi Serie C Iwapo unadhania timu yako imekuwa na msururu wa matokeo mabaya wikendi hii basi fikiria kichapo hiki walichopewa Pro Piacenza katika ligi ya Itali. Klabu hiyo ya ligi ya Serie C iliowekwa katika kundi A ilishindwa magoli 20-0, ' ndio magoli ishirini bila jibu ' na wapinzani wao katika ligi hiyo Cuneo siku ya Jumapili jioni. Walikuwa nyuma kwa magoli 16 kwa bila wakati wa muda wa mapumziko huku mshambuliaji wa Cuneo Hicham Kanis akifunga magoli sita pekee kabla ya mapumziko naye mshambuliaji mwenza Eduardo Defendi akipata magili matano. Katika safu ya ulinzi ya Pro Piacenza kulikuwa na matatizo yaliosababisha mvua hiyo ya magoli. Wakiwa chini katika ligi hiyo ya tatu ya Itali, klabu hiyo ya kaskazini ina matatizo makubwa ya ufadhili. Walipokonywa pointi nane mapema katika kampeni yao na wameripotiwa kushindwa kuwalipa wachezaji wao tangu mwezi Agosti hatua iliosababisha kujiuzulu kwa wachezaji wengi wa ki...

Ronaldo amchana Messi, amtaka abadilike

Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo ameibuka na kumzungumzia nyota wa Barcelona, Lionel Messi akisema angependa kumuona mchezaji huyo akicheza katika ligi kuu nchini Italia 'Serie A'. Cristiano Ronaldo na Lionel Messi Cristiano Ronaldo amemhimiza mpinzani wake huyo wa muda mrefu Lionel Messi, akimtaka  "kukubali changamoto" na kumfuata nchini Italia. Alipoulizwa kama anamuhitaji Messi au la!, Ronaldo amesema, " hapana, labda yeye ndiyo ananihitaji mimi. Nimecheza Ureno, Uingereza, Hispania, Italia na kwenye timu ya taifa pia, lakini yeye bado yuko kwenye timu moja. Labda yeye kama ananihitaji mimi ". " Kwangu mimi maisha ni changamoto, ninapenda hivyo na ninapenda kuwafanya watu wangu wawe na furaha. Ningependa siku moja nayeye aje kucheza Italia kama nilivyofanya mimi, akubali changamoto, lakini kama ana furaha pale alipo ninaheshimu uamuzi wake ", ameongeza Ronaldo. Aidha Cristiano amemzungumzia Messi kama ni mchezaji mkubwa...

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 21.11.2018: Eriksen, Rashford, De Jong, Kante, Perisic, Rabiot, Hernandez

Frenkie de Jong Manchester City watahitajika kulipa pauni milioni 75 kwa kiungo wa kati wa Ajax, Frenkie de Jong, ambaye pia anatafutwa na Barcelona. Mchezaji huyo wa miaka 21 pia anawinda na meneja wa City Pep Guardiola. (Mirror) Real Madrid wanapanga kutumia pauni milioni 90 kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 21, na paunia milioni 40 kwa kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 26. (Sun) Kiungo wa kati Mfaransa N'Golo Kante, 27, yuko tayari kusaibi mkataba mpya na Chelesea wa thamani ya karibu pauni milioni 300,000 kwa wiki. (Telegraph) N'Golo Kante Real Madrid wanajaribu kumshawishi kiungo wa kati mhispania Brahim Diaz, 19, asiongeze mkataba wake na Manchester City. (AS) Inter Milan wanafikitria ikiwa watamuuza wing'a raia wa Croatia Ivan Perisic, 29, kwenda Manchester United kwa paunia milioni 31. (Sun) Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, ameiambia Barcelona kuwa atajiunga na klabu hiyo msimu ujao. (Mundo Depo...

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano kuhusu uhamiaji

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano juu ya mpango wa uhamiaji, unaozitaka nchi wanachama kwa hiari kuanzisha vituo vya udhibiti kushughulikia wahamiaji waliookolewa baharini na kuanzisha vituo nje ya ulaya. Mpango huo wa maelewano uliofikiwa mapema asubuhi ya leo unakuja baada ya majadiliano yaliyodumu kwa muda wa masaa zaidi ya 12, wakati viongozi hao walipokutana katikati mwa ongezeko la shinikizo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo la uhamiaji, unaonekana kuhatarisha mustakabali wa umoja huo. Mpango huo ni ushindi kwa Italia, inayoongozwa na waziri mkuu Giuseppe Conte, ambaye amekuwa akisukuma ajenda ya kugawana mzigo wa wahamiaji miongoni mwa nchi wanachama na hata kutishia kutumia kura yake ya turufu katika maamuzi ya mkutano huo wa kilele hadi pale viongozi wake wangefikia makubaliano ya pamoja juu ya uhamiaji. "Kwa hiyo naweza kusema kwa ujumla tunaweza kuridhika. Yalikuwa majadiliano ya muda mrefu lakini kuanzia leo Italia haiko peke yake," alisema C...

Italia yatumbukia katika mgogoro wa kisiasa

Italia imetumbukia katika mgogoro mpya wa kisiasa baada ya kusambaratika kwa jaribio la vyama vinavyofuata siasa za kizalendo kuchukua madaraka. Hii ni baada ya Waziri Mkuu mtarajiwa Giuseppe Conte kujiuzulu Rais wa nchi hiyo Sergio Mattarella anatarajiwa kumteua mchumi anayeunga mkono sera za kubana matumizi kuiongoza serikali ya watalaamu kabla ya uchaguzi mpya. Rais Sergio Mattarella alitumia kura ya turufu kupinga uteuzi wa kiongozi anayekosoa vikali sera za Ulaya Paolo Savona kuwa waziri wa uchumi, hatua iliyovikasirisha vyama vya upinzani vya Five Star Movement na the League cha siasa kali za mrengo wa kulia na kusababisha waziri mkuu wao mteule Giuseppe Conte kujiuzulu. Conte, mwenye umri wa miaka 53, ambaye ni wakili asiye na ujuzi wa kisiasa alitangaza kuwa ameachana na juhudi zake za kuunda serikali ya mabadiliko, hatua iliyoitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa karibu miezi mitatu baada ya uchaguzi mkuu wa Machi ambao haukutoa mshindi wa wazi. "Kam...

Kansela Angela Merkel apokea tuzo ya 'Taa ya Amani'

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametunukiwa tuzo ya Fransisca ya ‘'Taa ya Amani". Bibi Merkel amepewa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuhamasisha ushirikiano na amani miongoni mwa watu. Wakati akipokea tuzo hiyo kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema njia ya amani na maridhiano mara nyingi hufaulu pale panapokuwa na jitihada na uvumilivu mwingi, na alisisitiza kuwa njia hiyo sio kizuizi cha imani ya kidini. Akitolea mfano matatizo katika Umoja wa Ulaya unaojumuisha mataifa 28, bibi Merkel amesema ni muhimu kuangalia mbali zaidi ya upeo wa kitaifa, na kuongeza kuwa ni lazima uwepo uwezekano wa kuupa moyo Umoja wa Ulaya. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Kansela wa Ujerumani alielezea juu ya amani na jinsi inavyoendelea kuwa dhaifu duniani, akitolea mfano vita vya Balkans, iliyokuwa zamani Yugoslavia kwenye miaka ya tisini.Pia alizungumzia hatua ya Urusi ya kulitwaa jimbo la Crimea  mnamo mwaka 2014 pamoja na vita vya hivi karibuni vya wenyewe kwa wenye...