Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WAZIRI MKUU

Mizengo Pinda azungumzia Upinzani

Mizengo Pinda azungumzia maumivu ya Upinzani Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameweka wazi jinsi alivyokuwa akiumizwa na kauli za upinzani dhidi ya uongozi wake na kusema kuwa anaushangaa upinzani kulalamikia uongozi ambao waliulilia kwa muda mrefu. Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda. Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma, Pinda amesema kuna kipindi wakati wa uongozi wake, wapinzani walikuwa wakiinyooshea kidole serikali yao kuwa ni dhaifu haina makali, hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uamuzi mgumu. " Kauli hiyo na ilikuwa ikinikera kwa sababu ilitulenga viongozi wa wakati ule, lakini sasa nashangaa kuona wapinzani haohao wameanza kulalamika tena juu ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa aina waliyekuwa wakitamani kumpata" , amesema Pinda. Pinda amesema kuwa, Rais Magufuli ndiye kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamhitaji kutokana na uthubutu alionao katika kutekeleza miradi ...

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda Wasanii kutumia mitandao kutangaza utalii

Picha za Amber Rutty zinaleta joto DSM" - Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wasanii kutumia mitandao ya Kijamii kuhamasisha masuala ya Utalii wa nchi ili waweze kuitangaza Tanzania kupitia wafuasi wao wa mitandao ya kijamii ambao wanapatikana nchi mbalimbali. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia), na Amber Rutty. Akizungumza Jijini Dar es salaam, mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Waziri Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, Makonda amewataka wasanii wapewe nafasi ya kutangaza utalii huo. Makonda amesema " niwaombe wananchi wa Dar es salaam tutumie fursa hii kutangaza utalii wetu, niwaombe wasanii wenye wafuasi mitandaoni watangaze utalii wetu hapa nchini ili dunia ifahamu kuliko kusambaza picha za Amber Rutty ambazo zinaleta joto kali na laana ". " Tunatamani Dar es salaam isiwe sehemu ya kupita bali iwe sehemu ya watu kukaa, kwa sababu tuna maeneo ya utalii, ikiwemo ghorofa la kwanza kujengwa Ta...

Waziri Mkuu Majaliwa awageukia watumishi wa Serikali

Na Rahel Nyabali, Tabora   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji  wote wa serikali kuwajibika kikamilifu kwa kusikiliza kero na kutatua changamoto kwa wananchi kwa kujituma.  Ameyasema hayo Wilaya ya Tabora Mkoani Tabora katika  jukwaa la fursa biashara na uwekezaji na kuwataka wakuu wa Wilaya na watendaji kuwajibika vilivyo kwa kusimamia shuguli za serikali kikamilifu.  "Nachukua nafasi hii kwa kuwakumbusha ili kila mmoja akawajibike kwa nafasi yake kwa kutambua furssa zilizoko mahali husika kwa lengo la kuinua uchumi wa mmoja mmjo na taifa kwa ujumla ili kufikia uchumi wakati ifikapo 2025, amesema Majaliwa.  Majaliwa amesema Mkoa wa Tabora unafursa nyingi za uwekezaji hasa katika kilimo kwa mazao ya biashara na chakula  kwa kutambua fursa hiyo mkoa huo utafanikiwa kuongeza pato la Taifa  "Mkoa huu una ardhi yenye rutuba unazalisha tumbaku kwa asilimia kubwa una asali alizeti na zao la korosho litaanza kupandwa muda Si mrefu h...

BREAKING: Rais Magufuli Kaagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, OCD, Mkuu wa Upelelezi, Mkuu wa Kituo Kyerwa Wasimamishwe Kazi

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kyerwa Justine Joseph, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kyerwa Everist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa Robert Marwa.  Viongozi hao wa Polisi wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika Wilaya ya Kyerwa pamoja na tuhuma nyingine.  Aidha,Rais Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mej. Jen Jacob Kingu na Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa endapo watabainika kuhusika katika magendo ya kahawa na makosa mengine kwa mujibu wa sheria.  Tuhuma dhidi ya viongozi wa polisi katika Wilaya ya Kyerwa zimebainika  wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Maja...