Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 20, 2026

Lebanon: Mwanachama wa ISIS Akamatwa kwa Kupanga Njama ya Kumuua Papa Leo XIV Wakati wa Ziara ya 2025

Picha
Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Lebanon imethibitisha kukamatwa kwa raia wa Syria anayedaiwa kuwa mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Islamic State (ISIS), anayetuhumiwa kupanga njama ya kumuua Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, wakati wa ziara yake ya kihistoria nchini Lebanon mwaka 2025. Mtuhumiwa anafahamika kwa jina la kivita kama "Al-Daamish". Kwa mujibu wa chaneli ya MTV Lebanon na ripoti za kiusalama, Al-Daamish si jina geni katika ugaidi. Aliwahi kuwa mpiganaji wa Nusra Front kabla ya kuhamia ISIS, ambapo alipanda cheo hadi kuwa Naibu Gavana wa Aleppo ndani ya kundi hilo. Inadaiwa alikamatwa na utawala wa Bashar al-Assad na kutumikia kifungo cha miaka mitatu. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Assad Desemba 2024 na kufunguliwa kwa magereza nchini Syria, alitoroka na kuingia Lebanon kinyume cha sheria. Njama ya Mauaji Ilipangwaje Vyanzo vya kiusalama vinasema kuwa baada ya kuingia Lebanon, Al-Daamish aliwasiliana tena na viongozi wake wa I...

KUSAYA AONGOZA MAPOKEZI YA NDEGE YA ATCL MUSOMA

Picha
Musoma, Mara- Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Ndugu Gerald Musabila Kusaya, leo Septemba 17, 2026 ameongoza mapokezi ya ndege ya abiria ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Musoma, ikiashiria kurejea rasmi kwa safari za abiria baada ya takribani miaka minane. Safari ya mwisho ya ndege ya abiria katika kiwanja hicho ilikuwa Machi 2018 ya Shirika la Precision Air, kabla ya kufungwa kupisha upanuzi na ukarabati.  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara wakati wa mapokezi hayo, Kusaya amesema kurejea kwa huduma hizo ni fursa muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Mara. "Kurejea kwa ATCL ni fursa muhimu kwa wananchi kutokana na mchango wa usafiri wa anga katika kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo pamoja na kukuza biashara, utalii na uwekezaji," amesema Kusaya.  Kusaya ametoa shukrani kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa wa kuboresha kiwanja hicho na kulipa fidia kwa wananchi 58 waliopisha ujenzi. Amewataka wananchi wa Mara na mikoa jiran...