Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BREXIT

Maoni: Malumbano ya Brexit yazidi London

Kama Uingereza itashindwa kufafanua kuhusu ni nani anayeongoza utaratibu na kutoa maamuzi muhimu kuhusu Brexit, Umoja wa Ulaya utalazimika kuendelea kusubiri tu. Kwanza, Waziri anayehusika na masuala ya Brexit David Davis alijiuzulu, kisha Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni na aliyeongoza kampeni za kuitaka Uingereza kujiondoa Ulaya Boris Johnson akafuata. Wanalivuruga jaribio la Waziri Mkuu Theresa May la kuishawishi serikali yake kukubali Uingereza kuendeleza mahusiano ya karibu na Umoja wa Ulaya baada ya Brexit. Kujiuzulu huko kulikoratibiwa kwa mawaziri hao wenye misimamo mikali kuhusu Brexit kunaitumbukiza serikali ya May katika mgogoro na kuvuruga matumaini ya Umoja wa Ulaya ya kuweza hatimaye kuanza, katika wiki chache zijazo, mazungumzo muhimu kuhusu makubaliano ya kutengana na mahusiano ya usoni kati ya Uingereza na umoja huo. Ni Ijumaa iliyopita tu ambapo May alijaribu, kulazimisha kuliunganisha baraza lake la mawaziri linalozozana. Lakini kama mambo yanavyokwend...

Uingereza yatakiwa kuweka bayana msimamo wake juu ya Brexit

Umoja wa Ulaya umeionya Uingereza kuwa muda unayoyoma wa kufikia makubaliano juu ya mpango wa kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit. Umoja wa Ulaya umesema Uingereza inapaswa kuhakikisha kuwa haijiondoi kwenye Umoja huo mwezi Machi mwaka ujao bila ya makubaliano, hatua inayoongeza shinikizo kwa Waziri Mkuu Theresa May. Lakini kwa upande wake msemaji wa May,  amesema kinachopewa kipaumbele kwa sasa ni kutekeleza jambo hilo kwa makini na sio kukimbizana na muda. Wanadiplomasia na maafisa mjini Brussels wamesema kumekuwepo na maendeleo kidogo katika majadiliano ya Brexit tangu siku ya mwisho ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, na kuanza kutilia mashaka iwapo Umoja huo na Uingereza wataweza kufikia hatua nyengine muhimu katika mkutano wao wa kilele utakaofanyika June 28 na 29. Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May "Tuna wasiwasi kwamba hakuna msimamo wa wazi kutoka kwa Uingereza, muda unayoyoma, tunahitaji kupiga hatua muhimu lakini hilo halijafanyika, ki...