Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Uingereza yatakiwa kuweka bayana msimamo wake juu ya Brexit

Umoja wa Ulaya umeionya Uingereza kuwa muda unayoyoma wa kufikia makubaliano juu ya mpango wa kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit.


Umoja wa Ulaya umesema Uingereza inapaswa kuhakikisha kuwa haijiondoi kwenye Umoja huo mwezi Machi mwaka ujao bila ya makubaliano, hatua inayoongeza shinikizo kwa Waziri Mkuu Theresa May. Lakini kwa upande wake msemaji wa May,  amesema kinachopewa kipaumbele kwa sasa ni kutekeleza jambo hilo kwa makini na sio kukimbizana na muda.


Wanadiplomasia na maafisa mjini Brussels wamesema kumekuwepo na maendeleo kidogo katika majadiliano ya Brexit tangu siku ya mwisho ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, na kuanza kutilia mashaka iwapo Umoja huo na Uingereza wataweza kufikia hatua nyengine muhimu katika mkutano wao wa kilele utakaofanyika June 28 na 29.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

"Tuna wasiwasi kwamba hakuna msimamo wa wazi kutoka kwa Uingereza, muda unayoyoma, tunahitaji kupiga hatua muhimu lakini hilo halijafanyika, kile kinachotupa sisi wasiwasi hasaa ni suala la Ireland Kaskazini ambapo tunatarajia  mchango mkubwa kutoka kwa Uingereza," alisema Waziri wa masuala ya Umoja wa Ulaya wa Ujerumani Michael Roth alipokuwa anawahutubia wenzake mjini Brussels.

Nchini Uingereza kwenyewe Waziri Mkuu Theresa May yupo katika wakati mgumu, huku wafuasi wa Brexit wakitaka kukatizwa kwa mahusiano na Umoja wa Ulaya na watu wengine wanaotaka kuwepo kwa mahusiano ya karibu ya Uingerezana na Umoja huo huku wakihimiza ushirikiano wa karibu wa kibiashara ili kupunguza mgongano wa kibiashara katika siku za usoni.

Hata hivyo msemaji wa May amesema wanafanyia kazi mawazo mawili ya ushirikiano baada ya  Brexit.

Chini ya ushrikiano wa kiushuru, Uingereza inaweza kukusanya ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini kwa niaba ya Umoja wa Ulaya na chini ya wazo jengine la mpango makhsusi wa ushuru wa forodha, wafanyabiashara waliyo katika orodha iliyokubalika wataweza kuvuka mipaka kwa msaada wa teknolojia inayojiendesha yenyewe.

Bendera ya Uingereza ikiwa pamoja na bendera ya Umoja wa Ulaya

Masuala mengine ambayo hayajasawazishwa yanajumuisha dhamana ya wataalamu kutoka nje, makubaliano juu ya ushirikiano wa usalama na biashara baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya ili kuhakikisha kuwa kuna mpango wa kufuatwa baada ya Brexit mnamoMachi 2019.

Waziri wa Australia Gernot Blumel amesema Ulaya imeweka wazi msimamo wake na anatumai kuwa serikali ya Uingereza wataingia katika majadiliano kamili, akizungumzia malalamiko ya muda mrefu ya Umoja wa Ulaya kwamba Uingereza haijaweka wazi azma yake kwa kina katika majadiliano yake juu ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...