Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema leo kuwa nchi za Ulaya zinapaswa kusaidia kuijenga Syria ikiwa zinataka wakimbizi warudi nchini mwao. Akizungumza pamoja na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel katika mji wa kusini mwa Urusi wa Sochi, Putin amesema ujenzi wa Syria haupaswi kuingizwa siasa. Urusi inapinga msimamo wa Umoja wa Ulaya kuwa nchi za Magharibi zitazingatia tu msaada wa kiutu lakini hazitatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Syria kama Rais Bashar al Assad atakataa kugawana madaraka na upinzani. Merkel amemtaka Putin kutumia ushawishi wake kwa Assad kumfanya aibatilishe sheria ambayo itawapokonya Wasyria mali zao kama watashindwa kuzidai mara moja. Putin alikutana na Assad jana mjini Sochi na kumhimiza achukue hatua za kutafuta suluhisho la kisiasa
Maoni