Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Switzeland yaahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania

Switzeland imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kusaidia sekta mbalimbali za Maendeleo hususan katika suala la afya, kuongeza ajira na kukuza ujuzi .

Hayo yamebainishwa wakati wa Mkutano uliofanyika Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango na Balozi wa Switzerland nchini, Florence Tinguely Mattli, uliojaili uhusiano kati ya nchi hizo mbili na namna ya kuboresha ushirikiano.

Katika Mkutano huo, Waziri Mpango amemuomba Balozi huyo kuangalia uwezekano wa kuwapa mafunzo madaktari Bingwa nchini ili kukidhi uhitaji uliopo hususan katika Jiji la Dodoma ambalo ndiyo makao Makuu ya Nchi na  idadi ya wakazi wake inaongezeka.

Pia amemuomba kufadhili mafunzo kwa watumishi wa umma ili kuwajengea uwezo katika kada mbalimbali lengo likiwa ni  kuongeza ufanisi kazini.

Aidha kuhusu suala la uboreshaji miundombinu ya Jiji la Dodoma, Waziri Mpango aliiomba Switzerland kuangalia uwezekano wa kufadhili miradi ya maendeleo katika sekta ya maji na mazingira.

 ā€œTanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na mifugo mingi Barani Afrika lakini ufugaji wa mifugo hiyo hauna ubora kwa kuwa Switzerland imeendelea katika Sekta ya Mifugo fursa ipo ya uwekezaji katika eneo hilo nchini,ā€ alisema Dkt. Mpango.

Amesema kuwa Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na umasikini hivyo ni vema washirika wa Maendeleo wakatambua kuwa hatua ambazo Serikali inazichukua zikiwemo za kupambana na wakwepa kodi na kuboresha mikataba zenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania  kwa kuhakikisha wananufaika na rasilimali nyingi zilizopo nchini na wawekezaji waweze kunufaika pia.

Waziri Mpango amesema kuwa Switzerland inashiriki kikamilifu katika  miradi ya Matumizi bora ya misitu hususani mkoani Morogoro, kuboresha ujuzi na kukuza ajira kwa Watanzania.

Kwa upande wake, Balozi wa Switzerland nchini, Florence Tinguely Mattli, amesema kuwa uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania umezidi kuimarika na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania  katika sekta mbalimbali za maendeleo huku akisisitiza suala la kuzingatia  uwazi na mazingira bora ya uwekezaji  kwa kuwa ni chachu kubwa ya kuvutia uwekezaji wenye tija kwa pande zote mbili


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...