Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SOUTH AFRICA

Afrika Kusini inajibu madai ya Marekani ya kupeleka silaha Urusi

Shutuma za Washington zinakatisha tamaa na kudhoofisha uhusiano wa pande mbili, Rais Cyril Ramaphosa amesema Afrika Kusini inajibu madai ya Marekani ya kupeleka silaha Urusi Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mjini Pretoria Machi 16, 2023. © PHILL MAGAKOE / AFP Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amepinga shutuma za mjumbe wa Marekani aliyedai kuwa Pretoria iliipatia Urusi msaada wa kijeshi huku kukiwa na mzozo wa Ukraine. Siku ya Alhamisi, Reuben Brigety, balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, aliviambia vyombo vya habari kwamba ana hakika kwamba Pretoria iliipatia Moscow silaha na risasi, ambazo alisema zilipakiwa kwenye meli ya mizigo huko Simon's Town, kituo kikuu cha wanamaji cha Afrika Kusini, kati ya Desemba 6. na 8, 2022. "Kupewa silaha kwa Warusi ni mbaya sana, na hatufikirii suala hili kutatuliwa, na tungependa Afrika Kusini [ianze] kutekeleza sera yake ya kutof...

Mamlaka nchini Kenya zawazuia marubani wanafunzi kutua nchini humo

Marubani wanafunzi wa Afrika Kusini, waliotengeneza ndege aina ya Sling 4, wamewasili Kilimanjaro,Tanzania, wakiwa njiani kuelekea kwenye kituo chao cha mwisho, jijini Cairo. Timu ya wanafunzi hao waliondoka Zanzibar siku ya Jumapili, baada ya kutumia siku kadhaa bila mafanikio kuzungumza na mamlaka za nchini Kenya ili waweze kutua jijini Nairobi. ''Mamlaka nchini Kenya wamesema hawajafurahishwa na njia zetu hivyo wakatuzuia kuingia,'' alisema kiongozi wa wanafunzi hao, Des Werner, Baba wa Megan Werner 17, mwanzilishi waU-Dream Global. ''Tunaweza kubadili njia lakini hatuna muda wa kufanya hivyo.Tunafikiri kama ni wagumu tusilazimishe kwenda. Hata hivyo ni nchi yao ndio inayokosa nafasi ya vijana wa nchini kwao kuzungumza na timu yetu kwa ajili ya kuwapa msukumo vijana wa nchini mwao.'' Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi yatua Zanzibar Wanafunzi kuendesha ndege kutoka Afrika Kusini mpaka Misri Marubani hao wataelekea Uganda siku ya Jumanne l...

Spika Ndugai ataja kosa kubwa analoshtakiwa Masele

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele, hawezi kukaidi tena agizo la kutakiwa kufika Kamati ya Maadili baada ya kuitwa na Spika huyo kwa mara ya pili. Spika wa Bunge Job Ndugai. Akizungumza na waandishi wa habari Spika Ndugai amesema suala la Bunge kumuita Masele halihusiani na matukio yaliyotokea Afrika Kusini bali ni kwa sababu ya mambo aliyofanya nyumbani. Spika Ndugai amesema " ameitwa kwa mambo ya hapa nyumbani ya utovu wa nidhamu, anaunganisha hilo na matendo anayoyafanya huko, lakini hatujamuita kwa mambo ya South Afrika Watanzania watulie baada ya muda zitaletwa bungeni kila mtu atasikia kuhusu anatuhumiwa nini na majibu yake yalikuwa nini na wataelewa kama ameonewa au hajaonewa ." " Stephen Masele hawezi kukaidi zaidi kwa sababu ni lazima arudi Tanzania, labda sababu awe mkimbizi na  akirudi Tanzania lazima aje Kamati ya Maadili, ni wito wa kisheria tunachomuitia ni tabia yake uchonganishi wa viongozi, kwa sasa hatu...

Waafrika Kusini waandamana kisa Makonda

Wananchi nchini Afrika Kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania, wakipinga kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kukataza vitendo vya ushoga na usagaji kwenye mkoa wake. Wananchi hao ambao idadi yao haikujulikana kwa mara moja, pia wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini. “ Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu, tunakutaka uwape hifadhi watu hawa  wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu ”, walisikika waandamani hao kwenye ujumbe wao. Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na...

Utafiti: Wanawake wa Rwanda na Kenya ndio wataishi muda mrefu zaidi Afrika Mashariki

Wanawake nchini Rwanda na Kenya ndio wanaotarajiwa kuishi muda mrefu zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mujibu wa takwimu. Umri wa wanawake kuishi Rwanda kwa sasa ni miaka 69.3 na nchini Kenya ni miaka 69.0. Hata hivyo, umri wa kuishi wa wanaume Uganda ndio ulioongezeka zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, ambapo umepanda kwa miaka 13.5. Nchini Tanzania, umri wa kawaida wa kuishi kwa wanawake kufikia mwaka 2016 ulikuwa miaka 66, ongezeko la miaka 10 ukilinganisha na mwaka 1990 kwa mujibu wa Utafiti wa Mzigo wa Maradhi Duniani mwaka 2016, ulioratibiwa na Taasisi ya Takwimu za Afya na Utathmini. Kwa wanaume, umri wa kuishi ulikuwa miaka 62.6 kufikia mwaka 2016 ukilinganisha na miaka 53.7 mwaka 1990. Kwa kiwango cha kadiri, umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kwa miaka kumi kufikia sasa tangu mwaka 1990. Nchini Kenya, umri wa kuishi kwa wanawake umeongezeka kutoka miaka 62.6 mwaka 1990 hadi miaka 69 mwaka 2016,...

Fahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa

Nchi nyingi barani Afrika ni kinyume cha sheria kulima, kuuza au kutumia bangi Lesotho Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho. Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini. Afrika Kusini Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa. Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilish...

Je, rais Zuma atang'atuliwa madarakani kufuatia mabadiliko ya uongozi wa ANC?

MTEULE THE BEST Image caption Jacob Zuma amekuwa Rais wa ANC kwa miaka kumi sasa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma inawezekana asimalize muhula wake wa mwisho madarakani baada ya chama cha ANC kumchagua Cyril Ramaphosa kama kiongozi wake mkuu. Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, Ramaphosa alikua rafiki wa karibu wa Zuma na hata msaidizi wake, lakini uhusiano wao umekua wa mashaka siku za karibuni. Ramaphosa anasema atapambana na rushwa jambo ambalo kwa Zuma limekua kama mzigo. Hivi ni vitu vichache ambavyo vinaweza kujitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2019: 1.Zuma kutimuliwa Image caption Muhula wa Rais Zuma kuiongoza Afrika Kusini unaisha mwaka 2019 Chama cha ANC kitapendelea kuona kiongozi mkuu wa chama akiwa pia Rais wa nchi, jambo ambalo kama litatokea litamfanya Zuma kuachia ngazi ama kutimuliwa. Hii itafungua njia kwa Ramaphosa kuchukua madaraka na kujaribu kurudisha imani ya wengi iliyopotea juu ya chama hicho kinachotuhumiwa na ufisadi, huku asilimia...

Cyril Ramaphosa ndiye kiongozi mpya wa chama cha ANC, Afrika Kusini

MTEULE THE BEST Image caption Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC nchini A-Kusini . Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama tawala cha ANC nchini A-Kusini . Ramposa ambaye alikuwa makamu wa rais wa chama hicho aliweza kumshinda mpinzani wake Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye ni waziri wa zamani na alikuwa mke wa rais Zuma kwa kura 2440 kwa 2161. Kwa sasa Ramaphosa ameoneka kuwepo kwenye nafasi kubwa ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2019. Cyril Ramaphosa akiri kuwa na mpenzi nje ya ndoa Hata hivyo Cyril Ramposa amekuwa kiongozi wakati ambao Afrika kusini inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinafanya mambo hayendi sawa katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika . Cyril Ramaphosa ni mtu wa aina gani? Cyril Ramposa alizaliwa tarehe 17 mwezi novemba mwaka 1952 mjini Soweto, ndio mwanasiasa tajiri zaidi Afrika Kusini ,utajiri wake unakisiwa kuwa ni dola milioni 450.Tangu ujana wake Ramposa alikuwa na ndoto ...

ANC inamchagua kiongozi mpya Afrika Kusini

MTEULE THE BEST Wagombea ni makamu wa rais Cyril Ramaphosa na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa Bw Zuma Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimewaidhinisha wagombea wawili kuwania kumrithi Rais Jacob Zuma katika uongozi wa chama. Wagombea hao ni makamu wa rais Cyril Ramaphosa na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa bwana Zuma. Kumekuwa na mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa kura. Uwaniaji madaraka umeleta mvutano mkubwa wa kisiasa, hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019. Rais Zuma ameonya kuwa chama kimo hatarini na kimo kwenye njia panda. ANC Zaidi ya wajumbe 5,000 wanashiriki katika mkutano wa siku nne katika ukumbi wa Expo Centre mjini Johannesburg. Kwa namna inavyoonekana, Bw Ramaphosa ana wafuasi 1,469 kulinganisha na 1,094 wa mke wa zamani wa Rais Zuma, Bi Dlamini-Zuma. Lakini wengi wanasema pale ambapo matokeo yatawekwa wazi, k...

Jacob Zuma asema mustakabali wa ANC upo katika tishio.

MTEULE THE BEST Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe. Zuma anajiuzulu kama mwenyekiti wa ANC baada ya kuhudumu kwa muongo mmoja Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anasema mustakabali wa chama tawala African National Congress upo katika tishio. Alikuwa anazungumza katika mkutano wa kumchagua mtu atakayemrithi kama kiongozi wa chama hicho. Rais Zuma amezungumza kuhusu haja ya kuwa na umoja ndani ya ANC, kinachotishiwa na kumeguka. Mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mizozo kuhusu nani anayestahili kuruhusiwa kupiga kura. Zuma amesema tuhuma kuwa serikali yake ilishinikizwa na maslahi ya wafanya biashara zitachunguzwa. Wagombea wakuu wanaopigiwa upatu kumrithi kama kiongozi wa chama hicho ni naibu rais, Cyril Ramaphosa, na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Nkosazana Dlamini-Zuma, mkewe Zuma wa zamani. Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa. Chama hicho tawala ki...

Ramaphosa, Dlamini-Zuma kuwania uongozi wa ANC

MTEULE THE BEST Chama tawala nchini Afrika kusini,  ANC kinafanya uchaguzi mwishoni mwa juma, unaoonekana kuwa mgumu, kumchagua mrithi wa kiongozi wake Jacob Zuma, ambapo mshindi  pia atakuwa na nafasi ya kuwa  rais mpya wa nchi hiyo. Chama  cha  ANC  kitamtangaza  mrithi  wa  rais  wa  sasa  Zuma kuwa  kiongozi  wa  chama  Jumapili (17.12.2017), kikikamilisha mpambano  mkali  wa  kuwania  uongozi  ambao unatishia  kukigawa chama  hicho  ambacho  kilianza  kama  vuguvugu  la  ukombozi miaka  105  iliyopita, ambacho  kimekuwa  madarakani  tangu mwaka  1994. Makamu  wa  rais Cyril Ramaphosa , mwenye  umri  wa  miaka 65, ambaye  kwa  kiasi kikubwa  anapendelewa...