Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Je, rais Zuma atang'atuliwa madarakani kufuatia mabadiliko ya uongozi wa ANC?

MTEULE THE BEST


Image captionJacob Zuma amekuwa Rais wa ANC kwa miaka kumi sasa
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma inawezekana asimalize muhula wake wa mwisho madarakani baada ya chama cha ANC kumchagua Cyril Ramaphosa kama kiongozi wake mkuu.
Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, Ramaphosa alikua rafiki wa karibu wa Zuma na hata msaidizi wake, lakini uhusiano wao umekua wa mashaka siku za karibuni.
Ramaphosa anasema atapambana na rushwa jambo ambalo kwa Zuma limekua kama mzigo.
Hivi ni vitu vichache ambavyo vinaweza kujitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2019:

1.Zuma kutimuliwa

Muhula wa Rais Zuma kuiongoza Afrika Kusini unaisha mwaka 2019
Image captionMuhula wa Rais Zuma kuiongoza Afrika Kusini unaisha mwaka 2019
Chama cha ANC kitapendelea kuona kiongozi mkuu wa chama akiwa pia Rais wa nchi, jambo ambalo kama litatokea litamfanya Zuma kuachia ngazi ama kutimuliwa.
Hii itafungua njia kwa Ramaphosa kuchukua madaraka na kujaribu kurudisha imani ya wengi iliyopotea juu ya chama hicho kinachotuhumiwa na ufisadi, huku asilimia 62 ya uwezo wa chama hicho ukiwa mashakani.
Lakini jambo hili linatajwa kuwa la hatari kwa sababu linaweza kusambaratisha chama.

Baadhi ya viongozi wakuu wa ANC akiwemo Rais mpya wa chama na katibu mkuu wake wanaweza pia kumtimua.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Rais kufukuzwa ndani ya chama , mwaka 2008 Rais wa wakati huo Thabo Mbeki alitimuliwa baada ya Zuma kuingia madarakani kama Rais wa chama.
Uamuzi wa kumfukuza Zuma unaweza kufanywa na kamati kuu ya ANC ambayo ina mamlaka makubwa ndani ya chama.

2.Zuma kujiuzulu

Rais wa zamani Thabo Mbeki alijiuzulu baada ya kupata upinzani mkali ndani ya chama
Image captionRais wa zamani Thabo Mbeki alijiuzulu baada ya kupata upinzani mkali ndani ya chama
Jambo jingine ambalo limetajwa na mchambuzi wa masuala ya siasa wa Afrika Kusini Somadoda Fikeni ni uwezekano wa viongozi wakuu wa chama kumshawishi Zuma kuachia madaraka.
''Viongozi wa ANC wanaelewa gharama watakazoweza kuzipata iwapo Zuma atakuwa madarakani mpaka uchaguzi ujao''alisema.
''Kuna uwezekano wa kupoteza kura nyingi ama kushindwa kabisa,'' Aliongeza.
''Kwa maana hiyo uongozi huo unaweza kuongea nae kwa amani na kumshawishi kuachia ngazi kwa manufaa ya chama'',alisema Fikeni.

3.Zuma kusalia madarakani.

ANC ni chama kikongwe zaidi Afrika Kusini
Image captionANC ni chama kikongwe zaidi Afrika Kusini
Kuna wale wanaoamini kuwa litakua jambo lisilo na busara kwa Ramaphosa kumfukuza ndani ya chama Rais Zuma kwa sababu inawezakusababisha mgawanyiko katika chama hicho zaidi na kuharibu mipango yao juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.
Badala yake wanaona ni vyema kwa Ramaphosa kujiimarisha zaidi na kuwa karibu na Zuma ili kuongeza nguvu ya kushinda uchaguzi wa 2019.
NI kipi kitakachotokea? bila shaka huu ni wakati mgumu kwa Zuma

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...