MTEULE THE BEST
Meneja wa West Ham United, David Moyes, amesema anaweza kufundisha timu yoyote dunia na anataka kuonyesha kama ana uwezo huo akiwa na klabu ya West Ham.
Tangu alipoteuliwa kuwa mkufunzi wa Wagonga nyundo wa London, Moyes, ameisaidia timu hiyo kutoka katika mstari wa timu zinazatakiwa kushuka daraja kwa kutokufungwa michezo mitatu.
"Nafikiri nina uwezo wa kufanya kazi hii katika klabu yoyote duniani na nina uhakika nitalifanya hili nikiwa na West Ham," alisema kocha huyo.
Moyes mwenye miaka 54, anajaribu kurudisha heshima yake baada ya kufanya vibaya alipoviongoza vilabu vya Manchester United, Real Sociedad na Sunderland.
West Ham kwa sasa iko nafasi ya kumi na tano katika msimamo wa ligi ya nchini England
Maoni