Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 18.12.2017

MTEULE THE BEST

David Luiz
David Luiz
Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya Ā£60m kutaka kumnunua beki wa Juventus Alex Sandro, 26, mwezi Januari. (Mirror)
Rais wa Barcelona naye alikutana na familia ya Antoine Griezmann katika juhudi za karibuni zaidi za klabu hiyo kutaka kumnunua mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid mwenye miaka 25. (Mundo Deportivo)
Chelsea nao wanamnyatia mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 25, na wanataka kumchukua Januari. (Mirror)
    The Blues wako tayari kumuuza beki wao wa kati kutoka Brazil David Luiz ambaye kwa sasa ana miaka 30. (Mirror)
    Mabingwa wa Italia Juventus pamoja na wenzao wa Uhispania Real Madrid ni miongoni mwa klabu ambazo zina hamu sana ya kumchukua Luiz. (Daily Mail)
    Alex Sandro
    Beki wa Brazil Alex Sandro
    Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, amekataa mshahara wa Ā£400,000 kila wiki kutoka kwa klabu moja ya China kwa sababu anataka sana kuhamia Manchester City. (Sun)
    Everton nao waliwatuma maskauti kumfuatilia beki kinda wa Charlton Ezri Konsa, 20, Jumamosi. (Liverpool Echo)
    Bayern Munich wameafikiana mkataba wa euro 15m (Ā£13.2m) kumchukua mshambuliaji wa Hoffenheim Sandro Wagner, 30, mwezi Januari. (Bild)

    Klabu gani ina wakati mgumu zaidi msimu wa Krismasi?

    Wamiliki wa Stoke wametiwa wasiwasi sana na matokeo mabaya ya klabu hiyo karibuni lakini bado wanaamini Mark Hughes anafaa kusalia kama meneja wao. (Stoke Sentinel)
    Liverpool hawatawasilisha dau kumtaka beki Virgil van Dijk iwapo Southampton hawatashusha thamani ya Mholanzi huyo wa miaka 26 ke kutoka Ā£70m. (Irish Independent)
    Virgil van Dijk
    Kiungo wa kati wa Swansea na mkufunzi msaidizi Leon Britton, 35, atachukua usukani kama meneja iwapo Paul Clement atafutwa. (Sun)
    Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, anataka aongezewe mshahara wake na kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Marca)
      Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Bastian Schweinsteiger, 33, amepokea ofa kutoka kwa klabu kadha za Bundesliga huku mkataba wake klabu ya MLS ya Chicago Fire ukitarajiwa kufikia kikomo. (Die Welt)
      Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang aliongeza mkataba wake kisiri katika klabu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja hadi mwaka 2021. (Kicker)
      Ronaldo
      Cristiano Ronaldo anataka wachezaji wa Barcelona waandalie klabu ya Real Madrid gwaride la heshima klabu hizo zitakapokutana katika El Clasico Jumamosi. (Marca)

      Maoni

      Machapisho maarufu kutoka blogu hii

      MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

      Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

      Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

      MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

      Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

      Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...