MTEULE THE BEST
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli leo Disemba 20, 2017 ameunda tume ya watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini katika wajumbe hao yupo Wakili Albert Msando
Magufuli amesema hayo leo kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kikao chake cha kwanza ambacho kimefanyika mjini Dodoma.
Aidha Magufuli amewataka watu ambao wanashikilia mali za chama hicho wajitokeze na kutoa ushirikiano kwa watu hao huku akiwasisitiza wanachama wa CCM nao kutoa ushirikiano ili mali zao zisipotee.
Maoni