Ruka hadi kwenye maudhui makuu

"Hatutaki yajirudie ya Idi Amin" - CHADEMA

MTEULE THE BEST

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekosoa kitendo cha CCM kuweka mgombea wake kwenye nafasi ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki wakati haikutakiwa kufanywa hivyo, na kusema kwamba kitendo hicho kitasababisha mgogoro wa kidiplomasia.






Kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka kwa chama hiko, imesema CCM imekiuka utaratibu wa Bunge hilo la kumtafuta Spika la kuliongoza kwa kumuweka mtu wao kwenye kinyang'anyiro, wakati kiutaratibu ilitakiwa Spika wa awamu hii atoke nchi ya Rwanda kulingana na mzunguko ambao ulikuwa unafuatwa, na kwamba kitendo hicho kinaweza kuleta migogoro itakayoathiri Jumuiya hiyo kama kipindi cha Idi Amin.

"Awamu hii Spika alipaswa kutoka Rwanda, lakini Tanzania kwa kuwa CCM imezoea kutokuheshimu sheria na kanuni zilizopo imemteua mbunge wake Adam Kimbisa kugombea nafasi ya Spika kinyume kabisa na kanuni za Bunge hilo, na huu ukiwa ni mwendelezo wa utamaduni wao wa kutokuheshimu sheria na kanuni, kitendo ambacho kinatishia ustawi na uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki", imeandika Taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa .."CHADEMA tunalaani kitendo hiki, CCM wajue kuwa watabeba lawama zote kama kutakuwa na mgogoro ndani ya Bunge la Afrika Mashariki ambayo unaweza kupelekea mgogoro wa kidiplomasia katika Jumuiya nzima kutokana na tabia yao ya kutoheshimu taratibu zilizowekwa. Ttunataka kanuni za EAC ziheshimiwe, kwani tunakumbuka matendo ya Idd Amin mwaka 1977 yalivyovunja Jumuiya hii, hatutaki yajirudie kamwe".

Isome taarifa yote hapa chini.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...