Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UN kupigia kura mswada kuhusu Jerusalem

MTEULE THE BEST

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatafakari kupitisha mswada unaosema mabadiliko yoyote ya hadhi ya  mji wa Jerusalem hayatakuwa na athari kisheria na yanapaswa kubadilishwa



Balozi wa Misri katika Umoja wa mataifa Abdellatif Aboulatta

Misri imesambaza mswada  huo Jumamosi (16.12.2017), na wanadiplomasia  wamesema baraza  huenda  likapiga kura kuhusiana  na  mapendekezo  hayo mapema  hata  Jumatatu.

Akijitoa  katika  mwelekeo wa  kimataifa , rais  wa  Marekani Donald Trump  mwezi huu alitangaza  kwamba  atautambua  mji  wa  Jerusalem  katika  mji  mkuu  wa  Israel  na kuhamishia  ubalozi  wa  Marekani  katika  mji  huo  kutoka  Tel Aviv, hatua  hiyo  imezusha maandamano  na  shutuma  kali.



Maandamano ya kushutumu hatua ya Marekani kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Mswada  huo  wa  azimio  uliopatikana  na  shirika  la  habari  la  AFP  unasisitiza  kwamba Jerusalem  ni  suala , "ambalo  linaamuliwa  kupitia  majadiliano"  na  kueleza "masikitiko makubwa  katika  uamuzi  wa  hivi  karibuni  kuhusiana  na  hadhi  ya  mji  wa  Jerusalem," bila kutaja  moja  kwa  moja  uamuzi  wa  rais Trump.

"Uamuzi  wowote  na  hatua  ambazo  zitaonekana  kubadilisha  hadhi, hali  na  jamii  iliyopo katika  mji  huo  mtakatifu  wa  Jerusalem  havitakuwa  na  athari  ya  kisheria, na  ni  batili  na ni  lazima  ubadilishwe," mswada  huo  umesema.

Wanadiplomasia  wanasema  wanatarajia  Marekani  kutumia  uwezo wake  wa  kura  ya turufu  kuzuwia  hatua  hiyo  wakati , wengi  kama  sio  wote , wajumbe  14  wa  baraza  la Usalama  wanatarajia  kuunga  mkono  mswada  huo  wa  azimio.



Maandamano Gaza kupinga hatua ya Marekani kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Pence kwenda Mashariki ya kati

Makamu  wa  rais  wa  Marekani  Mike Pence  atazuru  Jerusalem  siku  ya  Jumatano , akijitumbukiza   katika  mzozo  wa  moja  kati ya  suala  lenye  utata  kabisa   katika  mzozo kati  ya  Wapalestina  na  Israel.

Israel ilichukua  udhibiti  wa  sehemu  ya  mashariki  mwa  mji  huo  katika  vita  vya  mashariki ya  kati  mwaka  1967  na  inaliona  eneo  lote  la  mji  wa  Jerusalem  kuwa  mji  ambao haukugawanyika.



Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence

Wapalestina  wanaliona  eneo  la  mashariki  mwa  Jerusalem  kuwa  mji  mkuu  wao  wa hapo  baadaye.

Balozi  wa  Israel  katika  Umoja  wa  mataifa  Danny Danon "anashutumu  vikali" mswada huo , akipuuzia  kwamba  ni  juhudi za Wapalestina "kuandika  upya  historia."

"Hakuna  kura  ama  mjadala  utakaobadilisha  hali  halisi  kwamba Jerusalem ilikuwa  ama itakuwa  mji  mkuu  wa  Israel," danon  alisema  katika  taarifa.

Mswada  huo  wa  azimio  unatoa  wito kwa  nchi  zote kujizuwia  kufungua  balozi  zao   mjini Jerusalem, ukiakisi  wasi  wasi  kwamba  serikali  nyingine zinaweza  kufuata  kile  Marekani ilichofanya.



Rais Donald Trump wakati akitoa tamko la kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Mswada  huo  unataka  kwamba  mataifa  yote  wanachama  kutotambua  hatua  yoyote ambayo  itakwenda   kinyume  na  maazimio  ya  Umoja  wa  Mataifa  kuhusu  hadhi  ya  mji huo.

Maazimio  kadhaa  ya  Umoja  wa  mataifa  yanaitaka  Israel  kujiondoa  kutoka  katika  ardhi iliyokamata  wakati  wa  vita  vya  mwaka  1967 na  kusisitiza  haja  ya  kufikisha  mwisho kulikalia  eneo  la  Wapalestina


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...