MTEULE THE BEST
Bunge la Seneti la Marekani limepitisha mswada ambao ulidumu kwa kwa zaidi ya miongo mitatu.
Bunge la wawakilishi lilipitisha mswada huo mapema leo.Republican wana idadi kubwa ya wabunge nchini Marekani, hiyo ikitajwa kuwa sababu mojawapo ya kupitishwa kwake licha ya awali kupingwa na baadhi ya wabunge wa chama tawala.
Mswada huo sasa utarudishwa bungeni siku ya Jumatano kwa hatua za kuitambua na kuiidhinisha moja kwa moja.
Iwapo itapita kama ilivyotarajiwa, itakuwa mafanikio makubwa sana kwa Rais Trump tokea aingie madarakani.
Wakosoaji wanasema sheria hiyo itapendelea zaidi watu matajiri kuliko wale wa tabaka la kati ama la chini.
Lakini chama cha Republican kinasema sheria hiyo itawanufaisha watu wote.
Makamu Rais Mike Pence alitoa matokeo ya kura hizo.
Katika mswada huu, kura 51 zinasema ndio na 48 hapana.kwa maana hiyo mswada huu utapitishwa kuwa sheria,''alisema.
Haya yanatajwa kuwa mafanikio makubwa kwa chama cha Republican haswa baada ya kushinwa kuondoa mfuko wa afya wa Obamacare.
Kiongozi wa chama cha Democratic Chuck Schumer amesema chama cha Republican kimejiingiza kwenye mgogoro mkubwa ambao utawagharimu hususan kwenye uchaguzi mdogo wa mwakani.
Spika wa Bunge Paul Ryan alisema '' Leo tunawarudishia watu wa nchi hii fedha zao, hizi ni fedha zao kwa hakika!''
Mswada huo utapigiwa tena kura siku ya Jumatano kabla ya kusainiwa na Rais Trump na kuwa sheria kamili.
Mswada huo utapunguza makato ya kodi kutoka asilimia 35 mpaka 21kwa makampuni makubwa na kupunguza pia kwa watu binafsi
Maoni