Korea Kusini yaitaka Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi nchini humo
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
-
MTEULE THE BEST
Image captionRais wa Korea Kusini Moon Jae-In
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In ameitaka Marekani kuacha kwa muda mazoezi yake ya kijeshi nchini humo mpaka kumalizika kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika mapema mwakani.
Anasema hii itasaidia pia kuifanya Korea Kaskazini kutotilia shaka uwepo wa wanamichezo wake kwenye michuano hiyo.
Korea Kusini itakua mwenyeji wa michezo hiyo itakayofanyika katika mji wa Pyeongchang mwezi Februari ikiwa ni kilomita 80 kutoka mpaka wake na Korea Kaskazini.
Mapema Canada na Marekani ziliapa kuendeleza mazoezi hayo ili kuisukuma Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa Nyuklia.
Image captionVikosi vya jeshi la Korea Kusini na Marekani vikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na mpaka wa Korea Kaskazini
Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kufuatia mpango wa matumizi ya mabomu ya Nyuklia unaofanywa na Korea Kaskazini.
Michuano ya Olimpiki ya majira ya bariki inatarajiwa kuhusisha pia wanamichezo kutoka Korea Kaskazini jambo ambalo Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In anaeleza kuwa ni la kuimarisha uhusiano zaidi
SHERIA 17 ZA SOKA ======================= Mchezo wa soka ni moja ya michezo maarufu sana duniani na ni biashara kubwa sana katika ulimwengu wa michezo na ukitaka kuamini hili angalia makampuni yaliyowekeza katika kudhamini soka – ni makampuni makubwa makubwa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa. Kwa kuzingatia aina hii ya wadhamini, waendeshaji wa mchezo wa soka, wameweka kanuni na miongozo ya kufuatwa ili kuhakikisha kuwa wale wanaowekeza pesa zao wanaona thamani ya uwekezaji wao. Kwa hiyo soka kama ilivyo katika michezo mingine inazo kanuni na tutajadili kanuni moja baada ya nyingine kama zilivobainishwa katika muongozo wa FIFA unaojulikana kwa jina la Law of the Game. Sheria Namba 1: Dimba ============== NYASI - Dimba la soka litakuwa la nyasi asilia au bandia kulingana na kanuni za masindano na nyasi hizo lazima ziwe za rangi ya kijani. Kwa dimba la nyasi bandia na kama mchezo unaochezwa utakuwa wa kutambuliwa na FIFA, basi nyasi hizo bandia lazima zikidhi viwango maalumu ...
Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi. Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria. Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao. Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...
MTEULE THE BEST TUMSIFU YESU KRISTO WAPENDWA KATIKA BWANA!!! MADA YA LEO: KUMTUMAINIA MUNGU SOMO; zaburi 11:1-7 Kwake MWENYEZI-MUNGU nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia "ruka kama ndege mpaka mlimani" Maana waovu wanavuta pinde wameweka mishale tayari juu ya uta wawapige mshale watu wema gizani! Kama misingi ikiaribiwa mtu mwadilifu atafanya nini? MWENYEZI-MUNGU yumo hekaluni mwake takatifu ; kiti cha enzi cha MWENYEZI-MUNGU kiko mbinguni Kwa macho yake huwachungulia wanadamu na kujua kila kitu wanachofanya MWENYEZI-MUNGU hupima waadilifu na waovu huwachukia kabisa watu wakatili Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberti upepo wa hari ndiyo itakuwa adhabu yao MWENYEZI-MUNGU ni mwadilifu na apenda uadilifu watu wanyoofu watakaa pamoja naye NENO LA BWANA Unaruhusiwa kuchangia funguka tupate maoni yako MUNGU AKUBARIKI
Maoni