Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UBALOZI

TRUMP AVUNZA MKATABA KUMKERA BARACK OBAMA SIRI HADHARANI

Barua mpya iliyovuja yadai Trump amevunja mkataba wa nyukilia 'ili kumkera Obama' Rais Donald Trump ameachana na mkataba wa nyukilia wa Iran ili kumkera Barack Obama, hiyo ni kwa mujibu wa barua ya siri iliyovuja kutoka kwa aliyekuwa balozi wa Uingereza nchini Marekani. Sir Kim Darroch alielezea hatua ya Trump kuvunja mkataba huo kama "ubadhirifu wa kidiplomasia" kwa mujibu wa gazeti la Mail on Sunday. Gazeti hilo linadai kuwa barua hiyo iliandikwa baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Borris Johnson kuirai Marekani mwaka 2018 kusalia ndani ya makubaliano hayo. Barua hii mpya inavuja katikakipindi ambacho polisis nchini Uingereza wameonya juu ya uchapishwaji wa barua hizo. Barua ya kwanza kutoka kwa balozi huyo ambayo ilikuwa inakosoa utawala wa Trump ilivuja wiki moja iliyopita na kusababisha majibizano ya hasira baina ya Uingereza na Marekani. Majibizano hayo yamesababisha Sir Kim kujiengua kwenye wadhifa wake licha ya serikali ya ...

Tanzania yafungua ubalozi wake Israel, Mahiga aomba Israel ifungue ubalozi Dar es Salaam

Dkt Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel jijini Tel Aviv Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania. Afisi hizo za kibalozi zinapatikana katika mji wa Tel Aviv. Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alikuwa amemualika Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi nchini Tanzania badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya. Waziri Mahiga, akizindua ubalozi huo Jumanne, alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania. Alisema JKT baada ya lugha ya Kiswahili ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja ha...