Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 10, 2017

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 16.12.2017

MTEULE THE BEST Carlo Ancelotti atarudi Stamford Bridge kabla ya kuanza kwa msimu mpya Carlo Ancelotti ameshinda mataji ya ligi katika nchi nne, na ni meneja mwenza mwenye ufanisi mkubwa katika historia ya kombe la Ulaya Carlo Ancelotti atarudi Stamford Bridge na kuwa meneja wa Chelsea kabla ya kuanza kwa msimu mpya. (Daily Record) Winga wa Monaco Thomas Lemar, 22, anawindwa na Chelsea, wanaotayarisha makubaliano ya fedha na mchezaji ya mshambuliaji Michy Batshuayi. (Daily Mirror) Batshuayi, 24, anatarajia kuondoka Chelsea mwezi ujao kwa mkopo kupunguza hofu ya kupoteza nafasi yake katika kikosi cha Ubelgiji kitakachocheza katika kombe la dunia. (London Evening Standard) Mchezaji kiungo cha kati raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 28, ametemwa na mkufunzi wa Manchester United, Jose Mourinho baada ya kuzuka mzozo kati yao wakati wa tathmini ya mechi katika uwanja wa mazoezi mwezi uliopita. (ESPN) Mkufunzi huo wa ManUnited boss Mourinho ana nafasi ya kusajili wachezaji mw...

ECOWAS yajadili uchumi siasa na usalama

MTEULE THE BEST Mkutano huo unafanyika katika wakati ambapo eneo hilo la Afrika magharibi linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mashambulio ya wanamgambo, uharamia katika ghuba ya Guinea na suala la uhamiaji haramu Viongozi wa mataifa na serikali wa jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS wanakutana leo mjini Abuja nchini Nigeria kujadili changamoto za kiuchumi, siasa na usalama zinazozikabili eneo hilo. Mkutano huo unafanyika katika wakati ambapo enoe hilo la Afrika magharibi linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mashambulio ya wanamgambo nchini Nigeria, Niger, Mali na Burkina Faso, uharamia katika ghuba ya Guinea na suala la uhamiaji haramu kutoka Afrika kwenda Ulaya. Ufichuzi wa hivi karibuni kwamba wahamiji wengi wanaotoka Afrika magharibi wanauzwa katika masoko ya watumwa nchini Libya umezusha hasira kimataifa na kumetolewa wito kwa hatua kuchukuliwa kusitisha uhamiaji haramu kuelekea Ulaya. Baadhi ya wahamiaji, wengi wao kutoka Nigeria, Gh...

Austria imerudi katika utawala wa mrengo wa kulia

MTEULE THE BEST Sebastian Kurz (kulia) na Heinz-Christian Strache wa Freedom Party Austria inakuwa nchi pekee ya Uropa magharibi kuwa na chama tawala kilicho na misimamo mikali ya mrengo wa kulia Rais wa Austria, Alexander Van der Bellen ameidhinisha kuundwa serikali ya muungano kati ya chama cha kihafidhina People's Party na cha mrengo wa kulia Freedom Party. Austria inaelekea kuwa nchi pekee ya Uropa magharibi kuwa na chama tawala kilicho na misimamo mikali ya mrengo wa kulia. Hii inatokana na hatua ya kiongozi Sebastian Kurz wa chama cha conservative Austrian People's Party kuridhia ushirikiano na chama kidogo cha mrengo wa kulia Freedom Party kinachoongozwa na Heinz-Christian Strache, ambao wao wanaendeleza sera kali hasa dhidi ya wahamiaji. Bwana Kurz mwenye ana miaka 31 pekee, na kama mpango huu utafanikiwa atakuwa pia kiongozi wa serikali mwenye umri mdogo zaidi duniani. Kwa muda wa miezi miwili sasa bunge la nchi hiyo limekuwa likijadili vipi kuzuia u...

Palestina yazika wahanga, yailaani Marekani

MTEULE THE BEST Serikali ya Palestina imekataa wito wa Marekani kutaka sehemu ya Ukuta wa Magharibi katika Mji Mkongwe wa Jerusalem kubakia kwenye udhibiti wa Israel, huku maziko ya Wapalestina waliouawa kwenye maandamano wakizikwa Afisa wa ngazi za juu kwenye serikali ya Palestina, Nabil Abu Rudeineh, ameliambia shirika la habari la WAFA kwamba kamwe Wapalestina hawatakubali mabadiliko yoyote kwenye mpaka wa 1967 wa Jerusalem Mashariki. "Msimamo huu wa Marekani unathibitisha kwa mara nyengine kwamba utawala wa sasa wa nchi hiyo haupo kabisa kwenye suala la kupatikana amani na badala yake unataka kuuimarisha ukaliaji wa kimabavu," alisema. Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Marekani alisema kabla ya kuanza kwa ziara ya Makamu wa Rais Mike Pence kwenye mataifa ya Misri, Israel na Ujerumani, kwamba nchi hiyo haiwezi kuona "ni kwa namna gani Ukuta wa Magharibi usiwe sehemu ya Israel" hata ikiwa patakuwa na makubaliano baina ya Waisraeli na Wapalestina.  ...

Yanga kukutana na Polisi Tanzania

MTEULE THE BEST Mechi ya kirafiki iliyopangwa kuchezwa leo kati ya Yanga na Polisi Tanzania itachezwa kesho Jumapili Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Afisa habari wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema awali, mechi hiyo ilipangwa ichezwe hii leo ikiwa ni maalumu kwa kikosi hicho kuangalia nyota wake baada ya kufanya mazoezi. " Mechi tulipanga tucheze leo lakini tumeahirisha kwani hapo awali tulipanga ichezwe leo Uwanja wa Taifa lakini Uwanja huo nyasi zake zilikatwa na bado hazijaota na kuwa sawa ili ziwe rafiki kwa wachezaji hivyo tutacheza kesho katika Uwanja wa Uhuru, mashabiki wetu tunaomba wajitokeze ili kuangalia kikosi chao ambacho kinajiandaa na mashindano mbalimbali,   " amesema. Yanga inajiandaa na mashindano mbalimbali ikiwemo yale ya Kimataifa ambapo itaanza na St. Louis ya Shelisheli katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali na michuano hiyo pia, Yanga inajiandaa na michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kutimua vumbi mwishoni mwa m...

Ronaldo amfurahia Messi

MTEULE THE BEST Nyota wa klabu ya soka ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo, amesema anajisikia vyema kutimiza malengo yake kwenye ulimwengu wa soka na anafuraha kushindana na Lionel Messi kwa muda mrefu. Akifanya mahojiano na tovuti rasmi ya FIFA, Ronaldo amesema ndoto yake ilikuwa kuweka historia na kuacha kumbukumbu kwenye ramani ya soka na hicho kitu kimetimia akiwa ametwaa mataji mengi pamoja na mafanikio binafsi ikiwemo tuzo tano za Ballon d’Or. “Najisikia vizuri kutimiza malengo yangu, nilitamani sana kuweka historia kuacha jina langu kwenye vitabu vya soka, nimepata mafanikio mengi sana ngazi ya klabu na taifa, nafurahia kuwa mmoja wa wachezaji waliofanikiwa zaidi kama kuchukua tuzo tano sawa na Messi”, amesema Ronaldo. Ronaldo ameongeza kuwa katika maisha yake amefanya kitu anachokipenda zaidi ambacho ni kucheza soka na amefanikiwa sana na hiyo inamuhamisha kuendelea kufanya vizuri akiwa bado anapenda soka kwasababu utafika wakat...

Zitto awaumbua Msando, Kitila na Mghwira

MTEULE THE BEST Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema wanachama wa Chama hicho waliohamia Chama cha Mapinduzi (CCM) sio kweli wanaunga mkono juhudi za Rais bali ni kwaajili ya madaraka na ahadi walizopewa. Hayo ameyasema leo kwenye hotuba yake kwa Kamati Kuu Juu ya chama hicho juu ya Hali ya Siasa Nchini Tanzania. Mh. Zitto ameeleza kuwa hoja inayotolewa na wanachama wanaohama ACT Wazalendo ya kuunga mkono jitihada za Rais haina mashiko kwani walikuwa na nafasi ya kuunga mkono wakiwa ndani ya chama hicho. "Takribani watu wote wanaoondoka kutoka vyama vya upinzani kwenda chama tawala wanasema wanaunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Tawala katika uendeshaji wa nchi yetu. Hii sababu haitoshi kueleza maamuzi yao, hususani kwa wale wanaotoka chama chetu cha ACT Wazalendo", amesema Zitto. Kiongozi huyo wa Chama ameongeza kuwa Halmashauri Kuu ya Chama iliyooketi katika ukumbi wa Jeshi la Wokovu, Aprili, 2016 iliazimia masuala a...

Msigwa ataka achomewe nyumba yake

MTEULE THE BEST Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini kumchomea nyumba anayoishi pamoja na magari yake endapo atahama Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kuhamia CCM. Msigwa amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni kuuza hadi utu wa wapiga kura. Msigwa ameweka wazi kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka upande wa chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama na bila hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020. "Nikihamia CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu  na magari yangu. Sikuingia bungeni kwa sababu nataka ghela ila nimeingia kwa sabu kuna hoja kuna agenda na kozi kama chama tunapigania.  Mkome kabisa kunipigia simu mimi sina bei itakayonihamisha CHADEMA, " amefunguka Msigwa Akizungumzia kuhusu alivyokuwa akirubuniwa,...

CCM yampata mrithi wa Nyalandu

MTEULE THE BEST Kamati Kuu ya Halmashauri  Kuu  ya  Taifa  ya  CCM,  na  kwa  niaba  ya  Halmashauri Kuu  ya  Taifa  (NEC) imefanya  uteuzi  wa  mwisho  kwa  wanachama wa  CCMwatakagombea  katika  Uchaguzi wa Ubunge katika Majimbo matatu. Katibu Mwenezi wa NEC-Itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema kwamba katika kikao hicho kilichofanyika jana mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wa chama cha CCM ambaye pia ni Rais , Dkt. John Pombe Magufuli  kilipitia majina ya walio omba dhamana na kwa kuzingatia misingi ya maadili, uchapakazi, uwakilishi   bora na wenye tija kwa wananchi. Taarifa hiyo imesema kamati kuu imewateuwa  Monko  Justine  Joseph,  Mgombea  wa  CCM Jimbo la Singida Kaskazini,Ndg.  Damas  Daniel  Ndumbaro,  Mgombea  wa CCM Jimbo la Songea Mjini na Ndg....

Ramaphosa, Dlamini-Zuma kuwania uongozi wa ANC

MTEULE THE BEST Chama tawala nchini Afrika kusini,  ANC kinafanya uchaguzi mwishoni mwa juma, unaoonekana kuwa mgumu, kumchagua mrithi wa kiongozi wake Jacob Zuma, ambapo mshindi  pia atakuwa na nafasi ya kuwa  rais mpya wa nchi hiyo. Chama  cha  ANC  kitamtangaza  mrithi  wa  rais  wa  sasa  Zuma kuwa  kiongozi  wa  chama  Jumapili (17.12.2017), kikikamilisha mpambano  mkali  wa  kuwania  uongozi  ambao unatishia  kukigawa chama  hicho  ambacho  kilianza  kama  vuguvugu  la  ukombozi miaka  105  iliyopita, ambacho  kimekuwa  madarakani  tangu mwaka  1994. Makamu  wa  rais Cyril Ramaphosa , mwenye  umri  wa  miaka 65, ambaye  kwa  kiasi kikubwa  anapendelewa...

Mwenyekiti aseme hela ziko wapi - Polepole

MTEULE THE BEST Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Humphrey Polepole amevipiga kijembe vyama vya upinzani akimtaka mwenyekiti wa moja ya vyama hivyo kusema hela ziko wapi. Kupitia ukurasa wake wa “Twitter” Polepole amendika maneno hayo bila kufafanua ni mwenyekiti wa chama gani na hela za nini japo wafuasi wake wengi katika mtandao huo wamechangia mawazo wakitaja huenda ni hela za ruzuku. Mbali na hilo Polepole pia amesema kuwa kile alichowahi kukitabiri kuwa upinzani hawataweza kushindana na chama chake siku za baadaye kimeanza kutimia. Hii inatafsiriwa kama majibu kwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freman Mbowe ambaye hivi karibuni alitangaza chama chake hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge endapo Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) haitazifanyia kazi kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwezi Novemba mwaka huu. “Nalipata kuwaambia wataweka mpira kwapani, wakasubiri siku kadhaa na hatimaye imekuwa. Kwa...

Mbunge amtaja aliyetaka kumuua Lissu

MTEULE THE BEST Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chaha (CHADEMA) amefunguka na kutaja sifa za mtu ambaye alitaka kumuua Tundu Lissu na kusema mtu huyo alishindwa kutekeleza hilo kwa kuwa Mungu hakupanga Lissu aondoke kwa kipindi hicho. Marwa Ryoba amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa hospitali ya Nairobi Kenya na kusema kuwa Mbunge huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kutolewa risasi 16 mwilini.  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma, baadaye alisafirishwa na kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi ambapo mpaka sasa anapatiwa matibabu huko.

RICHMOND UKWELI WOTE HAPA ANGALIA VIDEO

MTEULE THE BEST UKWELI KUHUSU RICHMOND ANGALIA HAPA MPENZI WA MIELEKA ANGALIA HAPA ROMAN NA ENDERTEKER

Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania December 15 2017 kuanzia ya Dini, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

MTEULE THE BEST