MTEULE THE BEST
Rais wa Marekani Donald Trump ameliagiza shirika la anga za juu la Marekani kupanga tena kutuma binadamu kwenye Mwezi kwa mara ya kwanza tangu 1972.
Mpango huo utaangazia upelelezi wa muda mrefu pamoja na uwezekano wa kutumiwa kwa uso wa Mwezi, kwa ushirikiano na sekta ya kibinafsi.
Bw Trump amesema mpango huo utaweka msingi wa kuwezesha mwishowe kutuma watu sayari ya Mars, ingawa hakutoa tarehe ya ni lini hilo linapangiwa kufanyika.
Wachanganuzi wanasema juhudi zozote kama hizo zitahitaji Bunge la Congress kukubali kuongezea shirika hilo fedha zaidi.
Wabunge Marekani huunga mkono upelelezi zaidi anga za juu lakini hutofautiana kuhusu malengo na bajeti.
Mapema mwaka huu, China ilitangaza kwamba inajiandaa kutuma binadamu kwenye Mwezi kwa mara ya kwanza.
Bw Trump, akiidhinisha mpango huo wake mpya, alisema: "Sisi ndio tunaoongoza na tutaendelea kusalia kuwa viongozi, na tutaongeza hilo sana."
Hatua ya Bw Trump ilipendekezwa na Baraza la Taifa la Anga za Juu ambalo huongozwa na makamu wa rais Mike Pence.
Agizo la Trump limeenda kinyume na mpango uliowekwa na mtangulzii wake Barack Obama, wa kuangazia zaidi kutuma binadamu katika sayari iliyo karibu na dunia
Maoni