Korea Kaskazini inahitaji mafuta lakini vikwazo vinazidi kuilemea Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa amevunjwa moyo na China kufuatia ripoti kwamba iliruhusu mafuta kusafirishwa hadi nchini Korea Kaskazini . Katika Ujumbe wa twitter, bwana Trump alisema kuwa China ilionekana '' hadharani'' ikiruhusu mafuta hayo kwenda Korea Kaskazini . Amesema hakuwezi kuwa na suluhu ya kirafiki katika mgogoro wa Korea Kaskazini iwapo mafuta yataruhusiwa kusafirishwa hadi Pyongyang. China mapema ilikana kwamba kumekuwa na ukiukaji wowote wa azimio la Umoja wa mataifa la mafuta kati ya China na Korea Kaskazini . Wiki iliopita , Beijing iliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililoandikwa na Marekani ambalo lilishirikisha hatua za kupunguza kiwango cha mafuta kinacheolekea Korea Kaskazini kwa asilimia 90. Ujumbe wa twitter uliochapishwa na rais Donald Trump Vi...