Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hofu ya Urusi kukata nyaya za mawasiliano ya mtandao chini ya bahari


There are more than 545,018 miles of fibre cables under the sea - enough to wrap around the Earth almost 22 times


Afisa wa cheo cha juu wa jeshi nchini Uingereza ameonya kuwa Urusi inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kwa uchumi ikiwa italenga nyaya za mawasiliano ya mitandao zinazopitia chini ya bahari.





Sir Stuart Peach, mkuu wa majeshi, alisema kuwa nyanya hizo zinaweza kukatwa au kuharibiwa.





Madai hayo yanazua maswali kadhaa:





Hiki ni kitu Urusi inaweza kukifabnya?





Ni kitu gani kitatokea ikiwa itafanya hivyo au ikiwa mtu mwingine atafanya hivyo?





Nyaya hizo ni za kufanyia nini?





Zinatumiwa katika mawasiliano ya mitandao kati ya ya nchi tofauti na mabara.





Nyaya zote hizo 428 zinachukua umbali wa kilomita milioni 1.1 na kuzunguka dunia nzima.





Kiwango kikubwa cha data husambazwa kote duniani nchini ya bahari kwa nyaya na zingine hjuwa nyembamba kama karatasi.




Je Urusi inaweza kukata nyaya za mawasiliano za chini ya bahari?


Kwa bahati mbaya, huku teknoljia yao ikiwa inategemewa sana, nyaya hizo zinaweza kuharibiwa. Nyaya hizo hufunikwa na plastiki, lakini nyingi bado zina upana wa sentimita tatu.





Majanga ya asili yanaweza kuziharibu na au hata meli ikitia nanga. Hicho ndicho kilitokea katika bandari ya Alexandria nchini Misri na kusababisha kukatwa mawasiliano kati ya Ulaya, Afrika na Asia.





Ni kwa nini wakuu ya jeshi wana hofu?





Mwandishi wa masuala ya ulinzi wa BBC Jonathan Beale anasema kuwa hofu ya Urusi kuweza kukata au kuharibu nyaya za chini ya bahari inazidi kuongezeka.





Nyambizi za Urusi zinazidi kuonekana sana bahari ya North Atlantic, hasa eneo lililo kati ya Grenland, Iceland na Uingereza.





Marshal Peach anasema kuwa Uingereza na washirika wake wa Nato wanakosa nyambizi, meli na ndege za kufanyia ujasusi.




Marshal Peach anasema kuwa Uingereza na washirika wake wa Nato wanakosa nyambizi, meli na ndege za kufanyia ujasusi.


Ni kitu gani kitatokea ikiwa nyaya hizo zitakatwa?





Keir Giles ambaye ni mtaalamu wa masuala ya vita vya mawasiliano vya Urusi, anasema kuwa hilo halina uwezekano wa kutokea kwa sababu linaweza pia kuiathiri Urusi, lakini ni kitu ambacho pia Urusi inaweza kukifanya.





Na ikiwa itatokea kutakuwa na madhara makubwa.




Nyanya hizo zinatumiwa katika mawasiliano ya mitandao kati ya ya nchi tofauti na mabara.


Anasema kuwa watu hata hawatakuwa na uwezi wa kuingia kwneye mtandao wa Facebook.





"Biashara ya kimataifa na malipo ya mashirika ya fedha hufanywa kupitia nyaya za chini ya bahari. Madhara ya uchumi yatakuwa ni makubwa."





Anaamini Urusi inataka kufahamu na kuacha kutegea sana mitandao na kubuni njia zake mbadala na kutaka kufahami pia kuhusu ni kipi kitatokea ikiwa mawasiliano ya mitandao yatavunjika



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...