Ikiwa leo Wakristo duniani kote wanaadhimisha sikukuu ya Krismas, Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Chemba amewataka Watanzania kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa Amani na Upendo.
Waziri Mwigulu ambaye wizara yake ndio ina dhamana ya kusimamia amani na usalama wa raia na mali zao nchini ametoa salamu zake za sikukuu huku akiwakumbusha wananchi kuzingatia Amani.
Kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Mh Mwigulu ameandika, “Merry Christmass & Happy New Year, tusherekee kwa Amani na Upendo”.
Mbali na Waziri Mwigulu kusisitiza Amani kipindi hiki cha sikukuu, hivi karibuni pia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro aliwataka Watanzania kusherehekea sikukuu bila kuvunja sheria za nchi
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni