Mkufunzi wa Man United Jose Mourinho
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa dau la £300m alilotumia kuimarisha kikosi chake halitoshi baada ya timu yake kutoka sare ya 2-2 na klabu ya Burnley siku ya Jumanne.
Jesse Lingard alifunga katika dakika za lala salama kusawazisha, na sasa sare hiyo inaiwacha Man United ikiwa pointi 12 nyuma ya viongozi wa ligi ManCity.
''Tuko katika mwaka wa pili kujaribu kujenga timu ambayo unajua sio miongoni mwa timu bora duniani'', alisema raia huyo wa Ureno.
''Manchester City inanunua mabeki wa kushoto na kulia kwa gharama ya washambuliaji, aliongezea''.
Mourinho ambaye aliteuliwa kuwa mufunzi wa United mnamo mwezi Mei 2016 na kuvunja rekodi ya dunia alipomnunua kiungo wa kati Paul Pogba kwa kitita cha £89m, Eric Bailly kwa kitita cha £30m na kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kwa £26.3m.
Mwaka huu alimnunua Romelu Lukaku kwa £75m ,beki Victor Lindelof kwa £31m na Nemanja Matic kwa £41m.
''Kutumia £300m hazitoshi.Gharama ya vilabu vikubwa ni tofauti na vilabu vyengine''.
''Klabu kubwa za zamani huadhibiwa katika soko kutokana na historia hiyo.Vijana wanafanya kile wanachoweza kufanya na wanaendelea vyema''.
Mourinho aliulizwa iwapo alama nane katika mechi tano zinatosha kwa klabu kama Man United.
Alijibu: Unaposema klabu kama United , je nadhani Milan sio klabu kubwa kama sisi?Unadhani Real Madrid sio klabu kubwa kama yetu?.
''Najua klabu kubwa ni gani.Kitu kimoja ni klabu kubwa na chengine ni ni klabu kubwa ya soka. Ni vitu tofauti''.
''Unazungumzia kuhusu jukumu la kutaka kushinda ligi ya Uingereza, Tottenham haina jukumu kama hilo kwa sababu sio klabu yenye historia kama yetu. Arsenal haina jukumu la kushinda. Chelsea haina jukumu la kushinda. Unapozungumzia kuhusu vilabu vikubwa unazungumzia kuhusu historia ya klabu
Maoni