Maandamano baada ya rais wa zamani Peru kuachiliwa

MTEULE THE BEST

Kenji Fujimori announces the pardon to his father Alberto in hospital, 24 December
Maandamano baada ya rais wa zamani Peru kuachiliwa
Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amemsamehe rais wa zamani Alberto Fujimori katika misingi ya kiafya katika hatua ambayo imezua maandamano makali.
Fujimori, 79, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ufisadi alihamishwa kutoka gerezani kwenda hospitalini kutokana na sababu za kiafya siku ya Jumamosi.
Bw Kuczynski alikana kuwa kumsamehe kwake kulikuwa ni sehemu ya makubaliano ya chama chake kuzuia kura ya kutokuwa na imani naye.
    Polisi katika mji mkuu Lima walipambana na waandamanaji baada ya kuibuka kwa habari hizo.
    Hata hivyo wafuasi wa Fujimor ambaye aliongoza Peru kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2000 walisherehekea nje ya hospitali ya serikali ambapo alikuwa akipata matibabu.
    Anapendwa na baadhi ya rais wa Peru kwa kuwamaliza waasi wa Mao lakini wakosoaji wake wanamtaja kuwa mtawala wa kiimla

    Maoni

    Machapisho maarufu kutoka blogu hii

    ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

    MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

    KUMTUMAINIA MUNGU