George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia

MTEULE THE BEST

George Weah Leo atangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo



Mwanasoka maarufu George Weah ashinda urais Liberia

George Weah Leo atatangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo baada ya kuongoza kwa asilimia 61.5 kati ya kura asilimia 98.1 zilizohesabiwa.

Bwana Weah amemtangulia mpinzani wake Joseph Boakai kwa kura asilimia 60.

Anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hio kupata kiongozi kwa njia ya kidemokrasia.

baada ya matokeo kutangazwa.

"Ninazielewa umuhimu na majukumu ya kazi kubwa niliyokabidhiwa leo. Mabadiliko yanakuja."

George Weah ni nani?

Weah ni mwanasoka maarufu aliyecheza kwenye klabu za soka za juu Ulaya kama Paris St-Germain (PSG) na AC Milan, kabla ya kumaliza taaluma yake nchini Uingereza kwa kuwachezea kwa muda mfupi klabu za Chelsea na Manchester City.

Ni Mwafrika pekee aliyewahi kushina tuzo ya Fifa ya mchezaji bora duniani ya na tuzo ya Ballon D'Or.

Aliingia katika uwanja wa siasa baada ya kustaafu kucheza mwaka 2002 na sasa ni seneta katika bunge la Liberia


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU