Wasanii wa muziki wa dansi Nguza Viking 'Babu Seya' na mwanawe Johnson Nguza 'Papii Kocha' ambao kwa sasa wapo mapumzikoni wanahangaika kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili waweze kumshukuru.
Msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini Mzee King Kiki amefunguka na kusema kuwa wasanii hao Babu Seya na Papii Kocha kwa sasa wapo mapumzikoni na kuwa wanahangaika kupata nafasi ya kuonana na Rais ili waweze kumshukuru kutokana na kuweza kuwapa msamaha mnamo Disemba 9, 2017 uliowafanya kuwa huru baada ya kutumikia jela kwa zaidi ya miaka 10.
"Saizi Nguza na Papii wapo kwenye mapumziko lakini wanapaswa kurudi nyumbani Congo kwenda kutekeleza mambo ya kimila, hivyo hawapaswi kufanya jambo lolote lile kwa sasa mpaka wakamilishe hilo suala la kimila, ila kabla ya wao kuondoka tumekuwa tukiomba kama tunaweza kupewa nafasi ya kuonana na Mhe. Rais kumshukuru na kumpa ahsante itakuwa ni vizuri sana kabla ya wao kwenda nyumbani"alisema Mzee King Kikii
Babu Seya na mwanaye Papii Kocha waliachiwa huru na kutoka jela mnamo Disemba 10, 2017 baada ya kupata msahama wa Rais John Pombe Magufuli Disemba 9,
Maoni