MTEULE THE BEST
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier katika maadhimisho ya siku ya Krismas mwaka huu wa 2017, kutoka Kasri la Rais la Bellevue.
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier katika maadhimisho ya siku ya Krismas mwaka huu wa 2017, kutoka Kasri la Rais la Bellevue.
Mabibi na Mabwana,
Katika maeneo mengi ya nchi yetu hii leo kumetulia kuliko wakati wowote ule. Utulivu huo, ambao unashuhudiwa nchini kote katika kipindi cha X-Mas, wakati ambapo maduka hufungwa, usafiri wa umma kupungua, watoto, wazazi au mamabu na mabibi huchukuliwa kutoka vituo vya treni, huo ndiyo utulivu ambao tungependa kuwa nao katika siku zote za mwaka. Ni wakati wa kipekee katika kipindi chote cha mwaka. Wakristu miongoni mwetu wanahusisha wakati huu wa utulivu, na amani inayoahidiwa katika simulizi za X-Mas. Katika muktadha huo napenda kuwatakia na sisi sote, wakati wa X-Mas ambao unaweza kutuinua katika kipindi cha mwaka mzima.
Nafahamu bila shaka kwamba tunaweza tu kufurahia utulivu huu, ikiwa unaweza kutuokoa kwenye pilikapilika zilizoutangulia. Wakati huu unaweza tu kutuliwaza tunapoutafuta, kwa sababu siyo jambo la kawaida na la wakati wote.
Katika mwaka huu unaomalizika nimezunguka sana nchi yetu na kufika katika maeneo yanayotamani kila kitu - Lakini hakuna utulivu. Maeneo ambako hakuna tena kituo cha mafuta au maduka ya vyakula, na wakati huo mkahawa umefungwa, njia za kwenda kwa daktari zinazidi kuwa pana na basi la mwisho limeondoka. Kuna maeneo mengi ya aina hiyo mashariki kama ilivyo Magharibi mwa nchi yetu. Na kutoka maeneo hayo nimefahamu kwamba; Kuna kimya kinachoweza kugeuka kitisho. Kwa sababu kwa waliobaki, maisha yamekuwa magumu! Na nafahamu kabisa kwamba watu katika maeneo hayo wamekataa tamaa, na wanahisi kutengwa.
Rais wa Ujerumani Frank- Walter Steinmeier
Lakini pia nimekutana na watu wasiokubali kwamba utupu unaenea - ambao ukimya huu wanautia uhai. Nadhani - wawakilishi wa wengine katika eneo lililoko katika jimbo la Saxony. Watu wengi hasa vijana walikuwa wamenyamaza kimya kupita kiasi. Ni watu ambao nyumbani kwao kunawapa sababu ya kubakia au hata kurudi. Nimefurahishwa sana na raia wa mji huo na hata meya wao. Watu hawafanyi miujiza huko.
Fedha zinakosekana kama zinavyokosekana katika maeneo mengine. Lakini hilo halijawa kikwazo kwao. Ndiyo maana hivi sasa kuna mgahawa mpya uliojengwa na watu wa kujitolea na kituo cha kukutana mjini kati, ukumbi mdogo wa sinema uliotengenezwa kwa juhudi na raia, eneo la michezo lililojengwa na majirani na nyumba ambazo jamii ilichukuwa jukumu la kuzikarabati zisiwoze na kuzijenga upya familia za vijana.
Watu wa namna hiyo, ambao nimekutana nao huko Saxony na Mecklenburg-Vorpommern na vile vile Bayern na Lower Saxony, watu wa aina hiyo wanatia moyo, na wanapaswa kutiwa moyo. Na zaidi ya hapo wanastahili kusaidiwa kisiasa. Kwa sababu mifano midogo inakuwa muhimu katika muktadha mkubwa.
Inatuonyesha kuwa hatutegemei huruma ya mazingira ya wakati fulani. Wakati ujao siyo majaaliwa! Tunaweza kushinda unyonge na kutengwa kwa kiwango kikubwa na kidogo tunapofanya jambo pamoja, tunapoangalia siyo tu wajibu wa wengine, lakini pia tukatambua wa kwetu. Kuwajibika pia kwa ajili ya wengine, kama wanavyofanya mamilioni ya wanaojitolewa nchini Ujerumani, kunatupa hisia za kuwa nyumbani katika taifa hili. Na kwa hilo natoa shukuran kwa kila mmoja.
Nazungumzia haya kwa sababu nina uhakika kwamba tunayo sababu ya kujiamini. Katika miongo iliyopita tumefaulu kupita katika migogoro mikubwa ya mara kwa mara na kujirejesha upya. Tumesalia kuwa nchi ambamo mantiki ya kiuchumi na haki ya kijamii ndiyo kanuni za muongozo wa kisiasa. Na sisi ni taifa ambalo linayo nguvu na nia ya kuendeleza mshikamano na ukuaji wa pamoja. Kwa hayo mawili, yapo mengi ya kufanya bado.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais Steinmeier
Kwa karibu miaka 30 iliyopita, X-Mas ilikuwa inasherehekewa katika muktadha wa mshango na shauku juu ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin. Huo ulikuwa ni wakati usiyosahaulika kwetu sote, na kwa wengi ulianzisha pia mwelekeo wa mashaka. Lakini je, tukiangalia nyuma, hatujifunzi jinsi ilivyokuwa na maana kukutana na wakati huu wa kipekee bila hofu? Kuanguka kwa ukuta haukuwa muujiza wa X-Mas; ilikuwa kazi ya watu wenye ujasiri!
Tangia wakati huo dunia imeanza kutuzunguka. Tunaishi katika wakati ambao mara kwa mara unatukabili na mambo yayiotarajiwa. Mambo hayo yanatutia mashaka pia! Tunatamani kuendelea, tunamatamani kuwa na uhakika. Lakini ikiwa sisi binadamu hatukuwa na ujasiri na kujiandaa kwa yasiyotarajiwa, basi wachungaji wa Bethlehem wangegawanyika.
Na mwisho, siyo kila yasiyotarajiwa yatufundishe hofu. Hilo linahusu pia uundwaji wa serikali, ambao unasubiriwa katika namna isiyo ya kawaida. Napenda kuwahakishia kwamba, serikali inatekeleza majukumu yake kulingana na kanuni ambazo katiba yetu inaziainisha wazi kwa mazingira kama haya, japokuwa kanuni hizo hazikuwahi kutumiwa katika miongo ya hivi karibuni. Hivyo tuwe na imani.
Mabibi na Mabwana,
Kwa namna ya kipekee napenda kuwashukuru wale wanaowahudumia watu wanaoishi pekee yao, ambao wanakosa usalama wa kifamilia, wauguzi na manesi, lakini pia maafisa wa polisi, wanajeshi, na wote, ambao wanafanyakazi zao kokote wanakohitajika.
Mabibi na Mabwana,
Nawatakia X-Mas yenye baraka. Na pia napenda kufikisha salam zangu za X-Mas kwa watu walioko katika nchi yetu, ambao hawakukulia katika utamaduni wa X-Mas, wanaoamini katika dini nyingine au wasio na dini kabisa. Kwa wote ambao wanashuhudia wakati huu maalumu katika taifa letu. Hebu tuonyeshe kwamba kila mmoja wetu anamjali mwenzake!
Mimi na Mke wangu tunawatakia X-Mas njema na ya amani
Maoni