Hugo Santillan: Bondia wa Argentina afariki kufuatia majeraha aliyopata katika pigano Santillan alikuwa bingwa wa zamani wa uzani wa feather Bondia wa Argentina Hugo Santillan amefariki kutokana na majeraha aliyopata katika pigano , siku chache baada ya kifo cha bondia wa Urusi Maxim Dadashev. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 23 alizirai katika ukumbi siku ya Jumamosi baada ya pigano lake la ukanda wa WBC dhidi ya Eduardo Javier Abreu nchini Argentina kuisha kwa sare. Alipelekwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini akafariki siku ya Alhamisi. ''Lala kwa amani, Hugo Santillan'' ,alisema afisa wa ukanda wa WBC katika ujumbe wake wa Twitter. Santillan ni bondia wa pili kufariki kutokana na majeraha aliyopata katika ulingo wa ndondi wiki hii baada ya kifo cha Dadashev kuthibitishwa siku ya Jumanne. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 alipelekwa hospitalini akitokwa na damu katika ubongo baada ya pigano lake la IBF ukanda wa Welterwieght dhidi ya Subriel Ma...