Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ATLANTIKI

Aanza safari ya kuvuka bahari ya Atlantiki kwa kutumia pipa

Jean-Jacques Savin: Raia wa Ufaransa Jean-Jacques Savin ametumia miezi kadhaa kutengeneza pipa hilo katika chelezo kimoja kusini magharibi mwa Ufaransa Bwana mmoja raia wa Ufaransa ameanza safari ya kuvuka bahari ya pili kwa ukubwa duniani, Atlantiki, kwa kutumia pipa kubwa aliloliunda mwenyewe. Jean-Jacques Savin, mwenye miaka 71, ameanzia safari hiyo kutoka mji wa El Hierro uliopo kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania na anataraji kufika visiwa vya Caribbean ndani ya miezi mitatu. Pipa hilo linategemea nguvu ya msukumo ya mawimbi pekee kufanikisha safari. Ndani ya pipa hilo kuna sehemu ya kulala, jiko na stoo ya kuhifadhi vitu. Bwana Savin pia atakuwa anaweka alama katika safari yake ili kuwawezesha wataalamu wa bahari kuyafanyia tafiti zaid mawimbi ya bahari ya Atlantiki. Taarifa zote kuhusu mwenendo wa safari hiyo zinawekwa kwenye  ukurasa maalumu wa mtandao wa Facebook  na ujumbe wa mwisho umeeleza kuwa pipa lilikuwa linaenda vizuri. Katika mahojiano kwa...