Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NEW ZEALAND

Putin Azungumuzia shambulio la kigaidi New Zealand

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New  Zealand ni kuitikisa nchi hiyo Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New  Zealand ni kuitikisa nchi hiyo. Katika mkutano wake na wawakilishi wa jamii katika Crimea na Sevastopol, Putin amejadili mashambulizi ya kigaidi juu ya misikiti huko New Zealand. Putin alionyesha heshima yake kwa wale waliouawa katika shambulio hilo. "Lengo la mashambulizi makubwa ya kigaidi huko New Zealand ni kuitingisha nchi." alisema. Akionyesha kuwa vitendo vya kigaidi ni hatari kwa kila nchi, Putin amesema kuwa Urusi haitaruhusu mashambulizi hayo. Katika mji wa Christchurch, New Zealand, wakati wa sala ya Ijumaa, watu 50 waliuawa na gaidi aliyoshambulia misikiti miwili.

BANGI KUTUMIKA HADHARI SASA

Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi? Sehemu mbalimbali duniani mtazamo kuhusiana na matumizi ya mmea wa cannabis yaani bangi unabadilika kwa kasi. Serikali mpya ya Mexico ina mpango wa kuhalalisha matumizi ya bangi kama njia ya kujiburudisha, sawa na ilivyofanya utawala mpya wa Luxembourg. Wakati huo huo, viongozi wakuu nchini New Zealand, wanakusudia kuandaa kura ya maoni ya namna watakavyoshughulikia swala hilo. Jinsi maoni ya umma - na yale ya serikali- yanavyobadilika, ni dhahiri kuwa mataifa mengi yatafuata mkondo huo. Maswali yanayoibuka ni kwa namna gani nchi hizo zitadhibiti matumizi na usambazaji wa mmea huo? Ni nini hasa kinachopelekea mataifa mbalimbali katika kulegeza kamba kwenye sheria zake, au hata kuamua kuidhinisha ,matumizi ya bangi moja kwa moja? Vita dhidi ya mihadarati Ilikuwa mwaka 2012 ambapo Uruguay, ilipoandika historia kwa kuwa taifa la kwanza duniani kuruhusu matumizi ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha. Hatua hiyo, ...

Walevi waunda kisiwa New Zealand kukwepa marufuku

MTEULE THE BEST Watu hao waliunda kisiwa kwa kutumia mchanga katika juhudi za kukwepa marufuku Wakazi kadha wa New Zealand walitumia ubunifu wa hali ya juu katika kinachoonekana kuwa juhudi za kukwepa marufuku ya kunywa pombe maeneo ya umma. Maji yalipokupwa baharini, walitumia mchanga kuunda 'kisiwa' kidogo katika sehemu ambayo mto Tairua unamwaga maji yake baharini katika rasi ya Coromandel Jumapili alasiri. Kisha, waliiweka meza yao ya safari na kufungua chupa zao za vinywaji na kuanza kujiburudisha. Wakazi walifanya mzaha kwamba walikuwa kwenye "eneo la bahari la kimataifa" lisilomilikiwa na taifa lolote hivyo hawangeathirika na marufuku hiyo ya pombe. Watu hao walibugia vinywaji vyao hadi usiku mkesha wa Mwaka Mpya na kutazama fataki zikirushwa kuukaribisha mwaka mpya kwa mujibu wa tovuti ya New Zealand ya stuff.co.nz. Kisiwa chao bado kilionekana Jumatatu asubuhi. Marufuku dhidi ya unywaji pombe hadharani ilitangazwa Coromandel kipindi cha mwaka mpya na ...