Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New Zealand ni kuitikisa nchi hiyo
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New Zealand ni kuitikisa nchi hiyo.
Katika mkutano wake na wawakilishi wa jamii katika Crimea na Sevastopol, Putin amejadili mashambulizi ya kigaidi juu ya misikiti huko New Zealand.
Putin alionyesha heshima yake kwa wale waliouawa katika shambulio hilo.
"Lengo la mashambulizi makubwa ya kigaidi huko New Zealand ni kuitingisha nchi." alisema.
Akionyesha kuwa vitendo vya kigaidi ni hatari kwa kila nchi, Putin amesema kuwa Urusi haitaruhusu mashambulizi hayo.
Katika mji wa Christchurch, New Zealand, wakati wa sala ya Ijumaa, watu 50 waliuawa na gaidi aliyoshambulia misikiti miwili.
Maoni