Wakosoaji wa mapendekezo ya sheria mpya wanasema inalenga kuwazuwia wanamuziki kama Bobi Wine (pichani) kutoa maoni hasi juu ya maafisa
Serikali ya Uganda inapendekeza sheria inayoweka masharti kwa wanamuziki wanaotoa nyimbo mpya kuziwasilisha zichunguzwe kabla ya kutolewa.
Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema inalenga kuwazuwia watu kutoa maoni hasi juu ya maafisa ambao wanakerwa na umaarufu wa mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop Bobi Wine.
Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36- ambaye aligeuka na kuwa mpinzani wa kisiasa , ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amepata ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana kwa kuikosoa serikali kupitia nyimbo zake. Taarifa ya mapendekezo ya sheria ya kuweka masharti kwa wanamuziki nchini Uganda imepokelewa kwa hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi wakionyesha kutokubaliana na mapendekezo hayo.
Africa Facts Zone@AfricaFactsZone
Uganda's Government has made new outrageous and dumbfounding laws for musicians, because of Activist, Bobi wine who is also a musician and Lawmaker.
81
107 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @AfricaFactsZone
United African Diaspora@UAD_org
Is Uganda’s proposed censorship law just another way to curtail popularity for Ugandan MP & musician, Bobi Wine?
New law proposes all artists / filmmakers must:
obtain a licence
seek permission to perform abroad
submit song lyrics / film scripts to government for approval4
See United African Diaspora's other Tweets
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @UAD_org
Rais wa Uganda Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, amekuwa mamlakani tangu 1986, na anatarajiwa kugombea tena urais katika uchaguzi wa mwaka 2021. Naibu waziri wa masuala ya jinsia, kazi na maendeleo ya jamii Peace Mutuuzo, aliliambia shirika la habari la Reuters katika mahojiano kuwa sheria mpya za muongozo wa muziki na burudani tayari zimekwisha andikwa na zinatarajiwa kupitishwa na baraza la mawaziri mwezi Machi.
Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, amekuwa mamlakani tangu 1986, na anatarajiwa kugombea tena urais katika uchaguzi wa mwaka 2021
Mingoni mwa sheria hizo ni zile zinaweka masharti kwa wanamuziki, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha yakiwemo kumtaka msanii kuwasilisha maandishi ya ujumbe wa wimbo na maneno ya filamu na namna wimbo utakavyochezwa kwenye hadhira ili kufanyiwa uchunguzi.
Maudhui yanayoonekana kuwa na lugha ya matusi au kunakili kazi ya mtu mwingine, yatapigwa marufuku, alisema waziri Mutuuzo.
Wanamuziki pia watatakiwa kuomba idhini ya serikali kufanya tamasha zao nje ya Uganda.
"Kama taifa hatuwezi kuendelea kuendekeza lugha ya matusi . Hili ni jambo tunafahamu limekuwa likifanyika . Watu wanatunga nyimbo za matusi dhidi ya wengine ," alisema Mutuuzo.
Vikosi vya usalama mara kwa mara vimekuwa vikizuwia mikutano na maandamano ya wapinzani kuwapiga na kuwafunga mahabusu.
Marufuku:
Wanamuziki na wasanii wengine watatatakiwa kuwa na usajili wa serikali ili kupata kibali cha kazi yao na wanaweza kunyang'anywa ikiwa watakiuka sharia.
"Msanii au yeyote anayeburudisha hadhira ambaye anakiuka maagizo atapokonywa cheti ," kulingana na mapendekezo ya sharia hiyo yaliyoangaliwa na shirika la habari la Reuters.
Wakosoaji wa rais Museveni wanasema amekuwa akionyesha kushindwa kuwavumilia wakosoaji wake, na vikosi vya usalama mara kwa mara vimekuwa vikizuwia mikutano na maandamano ya wapinzani kwa kuwatawanya kwa gesi za kutoa machozi na hata kuwapiga na kuwafunga mahabusu.
John Segawa, muigizaji na muongozaji wa filamu ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa masharti mapya yanalenga kuwatisha wasanii wanaoikosoa serikali.
"Tunahakikishiwa vipi haki yetu ya uhuru wa kujieleza wa Katiba kama tunahitaji kuwasilisha kazi zetu kwa ajili ya kuidhinishwa?," alisema.
Mamlaka hivi karibuni zilizuwia matamasha yaliyopangwa kfanywa na Bobi Wine, ambaye ameishutumu serikali kwa kuazimia kupata mapato yake yatokanayo na kutokana na msimamo wake wa kuipinga serikali.
Wakili wa masuala ya haki za binadamu nchini Uganda Ladislas Rwakafuzi alielezea sharia hizo kama "hatua ya adhabu ya serikali " inayotolewa kwa ajili ya kutuma ujumbe kwa Bobi Wine na sauti nyingine za ukosoaji katika sekta ya muziki.
Si Uganda pekee ambako wasanii wamewekewa masharti ya kazi zao
Wasanii nyota wa Tanzania Diamond Platnumz na Rayvanny ni miongoni mwa wanamuziki ambao kazi zao ziliwahi kupigwa marufuku kwa muda na serikali
Nchini Tanzania la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mwaka jana liliwawekea marufuku wasanii wa Muziki wa Bongo Flava Diamond Platnumz na Rayvanny wamefungiwa kufanya onyesho lolote ndani na nje ya Tanzania.
Wasanii hao wawili walikuwa awali wametakiwa kuuondoa wimbo wao kwa jina 'Mwanza' kutoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini wimbo huo umeendelea kuwepo kwenye YouTube. Baadae baraza hilo liliwapa ruhusa ya kuendelea na matamasha hayo.
Wasanii nyota wa Tanzania Diamond Platnumz na Rayvanny sasa ruksa kufanya maonesho yao ya nje ya Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limeeleza kuwa wasanii hao wapo huru kufanya maonesho yao ya nje ya nchi, huku marufuku ya kutumbuiza ndani ya Tanzania ikisalia.
Diamond na wasanii kutoka kundi analolimiliki la Wasafi wanatarajiwa kupanda jukwaani mjini Embu Disemba 24, kisha jiji la Mombasa mnamo Disemba 26 kabla ya kuhamia visiwani Komoro ambapo watatumbuiza Disemba 28
Maoni