Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Indonesia

Miunganisho ya Ndege ya Kimataifa ya Urusi Inapanuka

Moscow Airport Indonesia itazindua safari za ndege za moja kwa moja hadi Vladivostok katika Mashariki ya Mbali ya Urusi, na njia za usafiri kuelekea miji mingine mikubwa nchini humo, ubalozi wa Indonesia huko Moscow ulitangaza Ijumaa.  "Tutafungua usafiri wa ndege wa moja kwa moja na Jakarta," Berlian Helmi, naibu mkuu wa misheni katika ubalozi wa Indonesia nchini Urusi, aliiambia Tass siku ya Ijumaa, akimaanisha mji mkuu wa Indonesia.  "Kwanza, tutafungua safari ya ndege kati ya Jakarta na Vladivostok, kisha kupitia Vladivostok hadi Moscow, [Jamhuri ya Urusi ya] Bashkortostan, Nizhny Novgorod na Tomsk," alisema.  Makubaliano yote ya lazima na upande wa Urusi tayari yamefikiwa, mwanadiplomasia huyo alisema.  Indonesia iko tayari kuanza safari za ndege hadi Vladivostok punde tu uwanja wa ndege wa eneo hilo utakapothibitisha kuwa uko tayari kuzipokea, aliongeza.  

Utafiti: Tanzania yaorodheshwa miongoni mwa nchi uchumi utakua kwa kasi zaidi duniani

Rais Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa Mei 3, 2018. Tanzania imeorodheshwa kuwa miongoni mwa mataifa ambayo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi kufikia mwaka 2026. Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo cha Chuo Kikuu cha Havard cha Marekani kinakadiria kwamba uchumi wa Tanzania utakuwa unakua kwa asilimia 6.15 wakati huo. Tanzania itakuwa ya nne kwa uchumi wake kukua kwa kasi Zaidi kufikia wakati huo. ADVERTISEMENT India ndiyo itakayoongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi ya 7.89 ikifuatwa na Uganda (7.46) na Misri ya tatu (6.63). Makadirio ya ukuaji ya kituo hicho yalifanywa kwa kutumia Mchangamano wa Kiuchumi, kipimo kimoja ambacho huangazia uchangamano wa uzalishaji na uchangamano wa uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kuuzwa nje katika taifa Fulani. Magufuli: Si wanafunzi wote watakaopewa mikopo Tanzania Magufuli: Wapuuzeni wanaodai se...

Kwa Picha: Watu walivyoukaribisha Mwaka Mpya wa 2018 miji mbalimbali duniani

MTEULE THE BEST Watu duniani waukaribisha mwaka 2018 kwa Sherehe Watu kote duniani wameukaribisha mwaka mpya wa 2018 kwa sherehe mbali mbali zikiwemo kufyatua fataki na kushiriki ibada maalum. Miongoni mwa nchi zilizoukaribisha kwanza mwaka huu mpya ni Australia ambako fataki ziliwashwa katika jengo maarufu la Sydney Opera.Hapa Ujerumani sherehe za kuukaribisha mwaka mpya zilifanyika chini ya usalama mkali kuepusha matukio ya uvunjaji sheria kama ilivyoshudiwa miaka miwili iliyopita ambapo wanawake walinyanyaswa kingono katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Cologne. Polisi mjini Berlin iliongeza askari 1,600 wa kushika doria.Hii leo Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ataendesha misa katika ukumbi wa Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican ambako atahimiza kuwepo amani duniani na kuhimiza ujumbe wa kuwajali wasiobahatika katika jamii hasa wahamiaji na wakimbizi. Ulimwengu unapoendelea kusherehekea kufika kwa mwaka mpya wa 2018, sherehe za aina yake z...