Rais Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa Mei 3, 2018.
Tanzania imeorodheshwa kuwa miongoni mwa mataifa ambayo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi kufikia mwaka 2026.
Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo cha Chuo Kikuu cha Havard cha Marekani kinakadiria kwamba uchumi wa Tanzania utakuwa unakua kwa asilimia 6.15 wakati huo.
Tanzania itakuwa ya nne kwa uchumi wake kukua kwa kasi Zaidi kufikia wakati huo.
India ndiyo itakayoongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi ya 7.89 ikifuatwa na Uganda (7.46) na Misri ya tatu (6.63).
Makadirio ya ukuaji ya kituo hicho yalifanywa kwa kutumia Mchangamano wa Kiuchumi, kipimo kimoja ambacho huangazia uchangamano wa uzalishaji na uchangamano wa uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kuuzwa nje katika taifa Fulani.
Magufuli: Si wanafunzi wote watakaopewa mikopo Tanzania
Magufuli: Wapuuzeni wanaodai serikali inakopa sana
Ripoti hiyo ya Havard ilibaini kwamba kampuni ambazo zimefanya mabadiliko chanya na kuingiza uchangamano katika sekta mbalimbali za uchumi kwa mfano India na Vietnam ndizo zitakazokua kwa kasi zaidi katika mwongo mmoja ujao.
Baada ya mwongo mmoja wa ukuaji wa kiuchumi ambao uliongozwa na mafuta na bei za bidhaa, watafiti wa Havard wamebaini kwamba mambo yamebadilika na sasa mataifa yenye uchumi unaotegemea sekta mbalimbali ndiyo yatakayofanya vyema Zaidi.
Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara, ukuaji wa kiuchumi ambao ulikuwa umeegemea mataifa ya magharibi mwa Afrika yaliyokuwa na mafuta pamoja na bidhaa sasa unaanza kuegemea zaidi Afrika Mashariki.
Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIAImage captionMuonekano wa daraja la Magufuli lililofunguliwa rasmi na Rais Magufuli Mei 5, 2018. Lina urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro
Baada ya Uganda na Tanzania, Kenya ni ya kumi katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kukua kwa kasi zaidi mwaka 2026 ambapo ukuaji wake utakuwa asilimia 5.87.
Mataifa 15 ambayo yanayokadiriwa kuongoza kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia 2026
NambariTaifaUkuaji wa Uchumi kwa %
1. India. 7.89
2. Uganda. 7.46
3. Egypt. 6.63
4. Tanzania. 6.15
5. Indonesia. 6.13
6. Kyrgyzstan. 6.04
7. Pakistan. 5.99
8. Vietnam. 5.89
9. Mali. 5.89
10. Kenya. 5.87
11. Philippines. 5.75
12. Madagascar. 5.73
13. Senegal. 5.7
14. Liberia. 5.7
15. Turkey. 5.57
Mataifa hayo ya Afrika Mashariki yameshuhudia wafanyakazi wake wengi wakiacha kilimo na kuingia kwenye sekta ya viwanda.
Bidhaa zinazouzwa nje kutoka mataifa hayo vimekuwa vikiongezeka, utafiti huo unasema.
"Kando na mabadiliko ya kuingia kwenye viwanda kuwa makubwa, yamekuwa yakifanyika polepole," utafiti huo unaonesha.
Sehemu ya ukuaji inatarajiwa pia kuchangiwa na ongezeko la idadi ya watu.
Wakati wa kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, kiongozi huyo alieleza matumaini kwamba uchumi wa Tanzania utatengemaa.
"Taifa letu linakwenda vizuri, uchumi wetu unakua vizuri, mwaka jana umekuwa kwa wastani wa asilimia 7 na mwaka huu tunatarajia utakua kwa wastani wa asilimia 7.1, mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 4," alisema
Maoni