Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Putin kuapaishwa kwa muhula wa nne kama rais wa Urusi


Putin alikuwa Sochi wiki iliyopita kutizama matayarisho ya kombe la Dunia wakati Urusi ndio mwenyeji

Vladimir Putin anatarajiwa kuapishwa kwa muhula wa nne kama rais wa Urusi leo Jumatatu baada ya kushinda uchaguzi mnamo Machi.


Amekuwa madarakani kwa miaka 18 kama rais na hata waziri mkuu, na wapinzani wameufananisha muda wake wa uongozi kama utawala wa mfalme.


Polisi wa kupambana na fujo walikabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wake mjini Moscow na katika miji mingine Jumamosi.


Kumekuwa na hofu kwamba huenda kutazuka ghasia tena leo Jumatau wakati anapoapishwa.


Sherehe hiyo ya kuapishwa kwake itafanyika Kremlin mjini Moscow na huedna ikawa na ya watu wa karibu tu ikilinganishwa na ile ya mwaka 2012, shirika la habari la AFP Linaripoti.


Putin anatarajiwa kukutana na watu waliojitolea kushughulika wakati wa kampeni yake peke, shirika hilo la habari linasema.

'


Rais wa kwanza aliyechaguliwa mnamo mwaka 2000, Putin aliwania tena muhula mwingine mnamo mwaka 2004 kabla ya kujiuzulu 2008 ili kuhudumu kama waziri mkuu chini ya mshirika wake Dmitry Medvedev, kwa sababu kisheria, anaruhusiwa kuhudumu kwa mihula miwili pekee mtawalia.


Ilikuwa wazi ni nani aliye na udhibiti na mwaka 2012 Putin alirudi kama rais, kwa mara hii kwa muhula wa miaka sita.


Iwapo na atakapofika mwisho wa muhula wake wa nne mwaka 2024, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 atakuwa amehudumu kwa takriban robo karne madarakani.


Jasusi aliyegeuka kuwa rais



Putin akiwa katika makao makuu ya ujasusi wa kijeshi GRU Moscow mnamo 2006

1952: Alizaliwa Octoba 7 huko Leningrad mji wa pili kwa ukubwa Urusi, akasomea Sheria na kujiunga na Polisi ya KGB akiwa jasusi katika Ujerumani mashariki iliyokuwa na Ukomyunisti


1997: Baada ya kuhudumu kama msaidizi mkuu wa meya wa St Petersburg, akaingia ikulu chini ya Boris Yeltsin akateuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha polisi FSB


1999: Alichaguliwa kuwa waziri mkuu , na kuwa kaimu rais baada ya Yeltsin kujiuzulu.


2000: Alichaguliwa Rais na kuhudumu mihula miwili ya miaka minne.


2008: Alizuiwa kuhudumu kwa muhula wa tatu mtawalia, akawashangaza wachambuzi kwa kurudi katika wadhifa wa waziri mkuu huku mshirika wake Dmitry Medvedev akiwa rais


2012: Achaguliwa tena rais na kwa muhula wa miaka sita, chini ya sheria mpya


2018: Achaguliwa kwa muhula wa nne


Urusi imebadilika vipi chini ya utawala wa Putin?


Warusi wa kawaida wamekaribisha utulivu unaotajwa kutokana na miaka ya kwanza ya uongozi wa Puti wakati mfumko wa bei ulidhibitiwa na idara msingi za serikali zilipofufuliwa.


Ghasia za kutaka kujitenga zilizogubika utawala wa kiongozi aliyemtangulia Putin, Boris Yeltsin, hatimaye zilisitishwa kwa umwagikaji damu mkubwa.



Putin na Bashar al-Assad katika ziara nchini Syria 2017

Umairi wake uliozidi ,uliochochewa na ushuru kutoka kwa mafuta gafi na gesi , Bw Putin aliongeza umairi wake uongozini na kusababisha vituo vya habari kurudia nyakati za kale pia uhuru wa kisiasa.


Uamuzi wake wa kuihamisha rasi ya annex Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 ulizua mgogoro mkubwa tangu vita baridi , na kusababisha vikwazo vinavyoendelea kutoka Magharibi hadi sasa.


Urusi inadaiwa kuingililia kati uchanguzi wa urais wa Marekani 2016 uliozua utata katika mahusiano ya kimataifa.


Mwaka huu Bw Putin aliitupiwa kidole cha lawama na Uingereza kwa shambulio la kemikali kwa jasusi wake - madai ambayo aliyapinga Moscow


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...