MTEULE THE BEST
Korea Kaskazini imewaachia huru raia watatu wa marekani kutoka gerezani, ukurasa wa tweeter wa Rais wa Marekani Donald Trump umeeleza.
hatua hiyo inaonekana kama dalili njema kuelekea mkutano wa kihistoria kati ya Rais Trump na mwenzie wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Bwana Trump amesema atawakaribisha watu hao watakaporejea na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo ambaye amekuwa mjini Pyongyang kufanya maandalizi ya mazungumzo hayo.
Kim Hak-song, Tony Kim and Kim Dong-chul walikuwa kifungoni baada ya kukutwa na hatia ya kufanya vitendo viovu dhidi ya serikali.
Rais Trump ametangaza kuachiwa kwao siku ya Jumatano.
''Afya yao inaonekana kuwa nzuri'', aliandika pia tarehe na mahali ambapo mazungumzo yatafanyika
Raia wa Marekani walioachiwa huru ni nani?
◾ Kim Hak-song alifungwa baada ya kushukiwa kutekeleza vitendo vya kikatili mwezi May mwaka 2017.Awali alijieleza juwa ni mmishenari wa kikristo aliyekuwa na nia ya kuanzisha shamba la majaribio katika chuo cha Sayansi na Teknolojia katika Chuo cha Pyongyang.
◾ Tony Kim, pia anajulikana kwa jina Kim Sang-duk, aliyefanya kazi kwenye chuo hicho pia, alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2017 kwa makosa ya ujasusi.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korea Kusini, alikuwa anafanya kazi na mashirika ya kibinaadam Korea Kaskazini.
◾ Kim Dong-chul, ni mchungaji aliye na miaka ya 60, alikamatwa mwaka 2015 kwa makosa ya ujasusi na akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani na kazi ngumu.
Mmoja wao alifungwa mwaka 2015, wengine wawili walifungwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, Kesi hizo zilikosolewa kuwa na misingi ya kisiasa na ukiukaji wa haki za binaadam.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Ripoti ziliibuka kuwa walitolewa gerezani na kupelekwa hotelini Pyongyang na kuibua hisia kuwa punde wataachiwa huru.
Ikulu ya Korea Kusini imeunga mkono kuachiwa huru kwa raia wa Marekani, ikisema ni ishara njema wakati wakielekea kwenye mazungumzo.
Msemaji wa Ikulu Yoon Young-chan pia ametoa wito wa kuachiwa kwa raia wao sita walioko kifungoni
Maoni