Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Marekani yajiondoa mkataba wa nyuklia na Iran

MTEULE THE BEST

Rais wa Marekani Donald Trump ameiondoa nchi yake kutoka kwa mkataba wa nyuklia kati ya Iran na mataifa ya magharibi, Jumanne (08.05.2018) akisema atavifufua tena vikwazo.

USA PK President Donald Trump zum Atomabkommen mit Iran (Reuters/J. Ernst)
Trump alisema mkataba huo umeoza kabisa kuanzia katika shina lake na anatumai kuafikiana makubaliano na Korea Kaskazini. Aliueleza mkataba kati ya Iran na nchi za Magharibi kuwa mbaya na unaoegemea upande mmoja.
Kauli ya Trump imekuja wakati alipotangaza mipango ya kuiondoa Marekani kutoka mkataba huo wa kihistoria na Iran wa mwaka 2015 wakati wa hotuba aliyoitoa kupitia televisheni katika ikulu ya mjini Washington. Trump alisema kama angeuruhusu mkataba huo kuendelea kuwepo, kungetokea katika siku chache zijazo mashindano ya silaza hza nyuklia. Pia alisema mkataba wa maana ungeeweza kuafikiwa wakati huo, lakini hilo halikufanyika.
Rais huyo wa Marekani ameieleza Iran kuwa "utawala wa ugaidi mkubwa". Trump amesema Wairan wanastahili serikali bora zaidi kuliko ile iliyopo madarakani. Na alisema "hakuna hatua iliyochukuliwa na utawala wa jamhuri hiyo ya kiislamu ambayo haijawa hatari zaidi kuliko kuendelea na mpango wake wa kutaka kumiliki silaha za nyuklia na njia za kuzisafirisha."
Nordkorea Mike Pompeo trifft Kim Jong Un (Reuters/U.S. Government)
Mike Pompeo, kushoto, alipokutana na Kim Jong Un wakati wa Pasaka Korea Kaskazini
Mshauri wa Trump wa masuala ya usalama wa taifa, John Bolton, alisema uamuzi wa Marekani unatoa ujumbe mzito kwa Korea Kaskazini kwamba haitakubali mkataba mbovu usiofaa.
Trump alisema waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Marekani, Mike Pompeo yuko mjini Tokyo nchini Japan, akielekea Korea Kaskazini na alitarajiwa kuwasili katika kipindi cha saa moja ijayo. Ziara hiyo inafanyika kabla mkutano uliopangwa kati ya Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un. Hi ni ziara ya pili ya Pompeo Korea Kaskazini. Trump alifichua mwezi uliopita kwamba Pompeo alikutana na Kim wikendi ya Pasaka mwaka huu. Trump alisema makubaliano yameafikiwa kuhusu siku na saa ya mkutano wake na Kim lakini bado anasubiriwa kutaja ni wapi atakapokutana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini.
Israel yaunga mkono hatua ya Marekani
Wakati haya yakirifiwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema anamuunga mkono rais wa Marekani kwa uamuzi wake wa kijasiri kujiondoa kutoka kwa mkataba wa nyuklia na Iran, ambao kiongozi huyo wa Israel amekuwa akiukosoa mara kwa mara.
Zypern Nikosia Benjamin Netanjahu, Nicos Anastasiades und Alexis Tsipras (Reuters/Y. Kourtoglou)
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kushoto, rais wa Cyprus, Nicos Anastasiades na waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras mjini Nicosia 08.05.2018
"Israel inaiunga mkono kikamilifu uamuzi wa rais Trump kuukataa mkataba wa maangamizi wa nyuklia," alisema Netanyahu katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni, akizungumzia mkataba kati ya mataifa ya magharibi na Iran, taifa ambalo ni hasimu mkubwa wa Israel.
Israel imewaamuru maafisa wake katika milima ya Golan kufungua na kuandaa maeneo ya kujificha kutokana na mashambulizi ya mabomu baada ya kutambua kile ambacho jeshi limekieleza kuwa ni "shughuli zisizo za kawaida za vikosi vya Iran nchini Syria". Tangazo hilo lilitolewa dakika chache kabla rais wa Marekani Donal Trump kutangaza kuiondoa nchi yake kutoka kwa mkataba wa nyuklia wa Iran wa mwaka 2015, hatua ambayo yumkini ikachochea hali ya wasiwasi katika kanda hiyo.
Kwa upande mwingine Saudi Arabia nayo pia imemuunga mkono rais Trump katika uamuzi wake. Hayo yameripotiwa na televisheni ya taifa ya Saudi Arabia. Televisheni hiyo pia imetangaza kwamba Iran ilitumia faida za kiuchumi ilizozipata baada ya kuondolewa vikwazo kuliyumbisha eneo zima la Mashariki ya Kati

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...