Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya A220-300

Baada ya kuwa gumzo Ghana sasa kutua Dar es salaam leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kuongoza mamia ya watanzania kupokea ndege ya kwanza kati ya ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania ambayo itawasili leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. Ndege hiyo itawasili leo majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo ilitua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege. Tukio la kupokea ndege hiyo litafanyika Uwanja wa ndege Mwalimu Julius Nyerere ambapo viongozi wengine mbalimbali wa nchi watawasili kushuhudia tukio hilo. Ndege hiyo A220 iliondoka Montreal Canada juzi saa 1:00 Jioni kwa saa za Canada na ikatua visiwa vya Santa Maria saa 5:00 usiku kwa saa za huko. Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus...

NDEGE YA TANZANIA AIR-BUS A220 YATUA ACCRA, KUTUA KESHO DAR ES SALAAM

Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini. Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.   Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege. Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220.   “Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona T...