Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BENKI KUU

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'

Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja. Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa. Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa. Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini. Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani. How could war with North Korea unfold? Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu...

TANZANIA YAIKOSOA BENKI YA DUNIA

Ni kwanini Tanzania imekosoa makadirio ya benki ya dunia ya ukuaji wa uchumi wake Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) Taasisi ya takwimu nchini Tanzania imesema kuwa inaweza kutathmini takwimu za ukuaji wa uchumi wake wa mwaka 2018 baada ya Benki ya dunia kutoa takwimu zilizoonyesha kiwango cha chini cha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo. Waziri wa fedha wa Tanzania aliliambia bunge mwezi uliopita kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilikuwa ni 7% mwaka jana. Benki ya dunia ambayo ilitoa hesabu zake kwa misingi ya data za taifa , matarajio ya mwaka 2019 ya ukuaji wa kiwango cha 5.4% - pia ilitoa kiwango cha chini cha ukuaji chini ya kile kilichokuwa kimekadiriwa na na serikali cha 7.1%. Albina Chuwa, mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ametetea njia zake na namna alivyofikia kiwango hicho, Reuters linaripoti. "Tumekwenda kote nchini kukusanya data halisi , sio sawa na mtu ambaye anakaa Washington na kutengeneza sampuli za pato la ndani ...

Benki ya TIB imetoa taarifa ya kusikitishwa

Benki ya TIB imetoa taarifa ya kusikitishwa kwake na kitendo cha dereva wa gari inayomilikiwa na benki hiyo yenye namba za usajili SU 38431 cha kubeba mbuzi kwenye tairi ya akiba iliyopo nyuma ya gari. Kwenye taarifa hiyo ambayo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Tawi la Mlimani City, imeeleza ni kwa namna gani dereva huyo ametumia mali ya umma vibaya, na pia kukiuka haki za wanyama. Benki hiyo imesema itamchukulia hatua stahiki dereva huyo, ambaye alikuwa akiendesha gari hilo kutoka Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.

Sababu zilizochangia benki tano kupigwa marufuku ya kubadilisha fedha za kigeni Tanzania

Noti za Tanzania Benki Kuu ya Tanzania imezipiga benki tano marufuku ya kuendesha biashara ya sarafu za kigeni kwa muda wa mwezi mmoja kwa kukiuka sheria kwa mujibu wa maafisa wa vyeo vya juu. Marufuku hiyo inakuja baada ya Benki Kuu kufanya ukaguzi wa ghafla kwenye maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kwenye mji ulio kaskazini wa Arusha kituo cha utalii na bishara ya madini. Kwa sasa kuna zaidi ya benki 40 zinazotoa huduma kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Kwa nini zimepigwa marufuku? Benki ya Barclays Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank zote zilipigwa marufuku ya kuendesha biashara hiyo Novemba 23 kwa kukiuka sheria za biashara, kwa mujibu wa Alexander Ng'winamila, mkurugenzi wa masoko ya fedha katika benki kuu. "Benki zilizopigwa marufuku aidha zilifanya biashara nje ya viwango vya masoko au hazikuwasilisha kwa Benki Kuu rrekodi za biashara zao, suala ambalo ni kinyume na sheria," Ng'winamila aliliambia shirika la Reuters. Barc...