Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'












Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini

Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (Ā£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja.



Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa.

Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa.


Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili

Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini.

Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani.



How could war with North Korea unfold?

Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, inasema Pyongyang "ilitumia uhalifu wa hali ya juu wa kimtandao kuiba pesa kutoka kwa taasisi za kifedha na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-kukusanya mapato yake".

Wataalamu pia wanachunguza shughuli za kimtandao zinolenga malipo kupitia fedha za kigeni.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa shambulio la Korea Kaskazini dhidi ya sarafu ya crypto- imeisaidia "kukusanya fedha kwa njia ambazo ni vigumu kutambuliwa na ikilinganishwa na ukaguzi wa kawaida unaofanywa na sekta ya benki".





Pia inasema Korea Kaskazini imekiuka vikwazo vua Umoja wa Mataifa kwa kutumia njia haramu ya kubadilishana fedha pamoja na kupata vifaa vya kutengeneza silaha ya maangamizi.

Tangu mwaka 2006, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa iliiwekea Korea Kaskazini vikwazo vya kuuza nje ya nchi hiyo bidhaa kama vile mkaa wa mawe, vyuma na vyakula vya baharini.

Pia iliwekewa kiwango cha uagizaji kutoka nje mafuta na bidhaa zake.


Kim Jong-un akifuatilia shughuli ya kufanyia majaribio makombora ya nchi yake

Kwa nini Korea Kaskazini inajaribu makombora?

Taarifa ya kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini inaeleza kuwa ushirikiano wa kijeshi baina ya Kusini na Marekani unawalazimu kuendelea kufanya ugunduzi na majaribio ya silaha mpya.

"Tunalazimika kuendelea, kujaribu na kutumia makombora mazito ambayo ni muhimu kwa kujilinda," imeeleza taarifa ya Kaskazini.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa kinachoendelea baina ya Marekani na Korea ya Kusini ni uvunjwaji wa wazi wa mazungumzo ya hivi karibuni baina ya Marekani na Korea Kaskazini (DPRK).


Helikopta za Marekani pia zinahusika katika mazoezi ya kivita Korea Kusini

"Tumeshaonya mara kadhaa kuwa mazoezi ya kivita yatazorotesha mahusiano baina ya Marekani na Korea Kaskazini na mahusiano ya Korea zote mbili kwa ujumlana kutufanya tufikirie kurejea tena hatua zetu za awali," inaeleza taarifa ya Kakazini.

Kwa mujibu wa jeshi la Kusini, makombora yaliyorushwa siku ya Jumanne ni ya masafa mafupi yanayoenda mpaka kilomita 450.

Ndani ya wiki mbili zilizopita, Kaskazini imekuwa ikirusha aina mpya ya makombora ya masafa mafupi.

Ijumaa iliyopita ilirusha makombora mawili yaliyoangukia kwenye bahari ya Japani.


Marais Trump na Mr Kim mjini Hanoi, Vietnam

Kim Jong- un mwaka jana wakati wa mkutano wake na rais wa Marekani Donald Trump nchini Singapore alikubali kuwa atakomesha kufanyia majaribio silaha za nyuklia

Kim pia alikubali kuwa Korea Kaskazini haitarusha tena makombora ya masafa marefu.

Mkutano wa pili kati ya viongozi hao Hanoi, mwaka jana ulimalizika bila makubaliano yoyote.

Kutokea wakati huo mazungumzo ya nyuklia yamekwama japo pande zote mbili zimeonesha juhudi ya katatua suala hilo kwa njia ya kidiplomasia


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...