Maelfu walikusanyika kwenye mkutano wa Waziri mkuu Abiy Ahmed Maafisa nchini Ethiopia wamesema kuwa watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa, baada ya mlipuko wa bomu kutokea kwenye mkutano wa kisiasa wa Waziri mkuu, Abiy Ahmed. Bwana Abiy amelitaja shambulio hilo kuwa ''jaribio lililoshindwa la vikosi ambavyo havitaki Ethiopia iungane''. Kiongozi huyo aliondolewa mara tu baada ya mlipuko, unaoelezwa wa guruneti linaloaminika kurushwa kati ya maelfu ya watu katika viwanja vya Meskel , mjini Adis Ababa Naibu mkuu wa Polisi mjini humo anashikiliwa kutokana na kushindwa kusimamia hali ya usalama katika eneo hilo. Maafisa wa polisi wanane wanashikiliwa na wakihojiwa kwa kushindwa kulilinda eneo lilofanyiwa mkutano Waziri wa afya nchini Ethiopia aliandika kwenye akaunti yake ya twitter kuwa watu wawili wamepoteza maisha na wengine 44 wako hospitalini, watano kati yao wakiwa na hali mbaya sana. Abiy alikuwa Waziri Mkuu baada ya...