MTEULE THE BEST
Katika siku ambayo baraza la usalama la Umoja wa mataifa linapiga kura kuidhinisha vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea kaskazini, kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-un, amesema taifa lake linawakilisha tishio kubwa la nyuklia kwa Marekani.
Katika hotuba iliyoripotiwa na shirika la utangazaji habari nchini (KCNA) Kim amesema kuendelezwa kwa haraka kwa mpango wa nchi yake wa nyuklia kunashinikiza ushawishi muhimu katika siasa za kimataifa.
- Kim Jong-un aahidi kurusha makombora zaidi Pacific
- Trump: Ningependa kukutana na Kim Jong-un
- Trump na Kim Jong-Un waitana ''wenda wazimu''
Azimio la hivi karibuni la baraza hilo la usalama katika Umoja wa mataifa linalenga kupiga marufuku usafirishaji wa bidhaa zote za mafuta kwenda Pyongyang na kuitisha kurudishwa kwa raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika nchi za nje katika muda wa mwaka
Maoni