Ruka hadi kwenye maudhui makuu

DCI azungumzia tukio la Lissu na Ben Sanane

MTEULE THE BEST


Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), amefunguka na kusema wao wanaendelea na upelelezi juu ya taarifa ya kutekwa kwa Ben Saanane na kudai hawawezi kusema kila hatua wanayochukua pia amedai polisi wanachukulia 'serious' shambulio la Lissu






DCI Boaz amesema hayo leo Disemba 20, 2017 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa amepata taarifa juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na kudai hawawezi kuwa wanatoa taarifa kwa kila hatua ambayo wamefikia. 

"Tumepata taarifa za huyo mwandishi kupotea na kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea zipo taratibu ambazo tunapaswa kuzichukua sisi kama polisi, suala la Ben Sanane tumeshalisema sana sisi kama upepelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua hairuhusiwa kisheria na katika kanuni zetu za upelelezi lakini niwathibitishie kwamba kila hatua inayostahili kufanywa ili kutrace mtu imeshafanyika" alisema DCI Boaz

Mbali hilo DCI aligusia kuhusu shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kusema kuwa jeshi la polisi linachukulia tukio hilo la kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu akiwa mjini Dodoma 'serious' 

"Jeshi la polisi linachukulia tukio hilo 'Serious' na sisi hatuwezi kujibishana na watu kwenye magazeti tunachukua hatua zote ambazo zinatuwezesha kutambua nani alitenda tukio hilo" alisema DCI Boaz


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...