Jonjo Shelvey
Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 26, hatajumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki kombe la dunia kutokana rekodi yake mbaya kinidhamu. (Mirror)
Manchester United wako tayari kuilipa Napoli pauni milioni 44 kumpata beki Elseid Hysaj msimu huu. Raia huyo wa Albania wa umri wa miaka 24 atakuwa mlinzi namba saba ghalia zaidi duniani. (Sun)
Everton watamfuta meneja Sam Allardyce saa 48 zinazokuja na wanakaraibia kumteua aliyekuwa meneja wa Watford Marco Silva. (Mirror)
Sam Allardyce
Afisa mkuu mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis na mkrugeni mkuu Josh Kroenke wamemtambua kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ambaye sasa ni kocha huko Manchester City kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri bado anaweza kuwa meneja wa Arsenal ikiwa atashinda vita vya kuhama wachezaji. (Star)
Arsenal: Pierre-Emerick Aubameyang
Mshambulizi wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang anasema alijiunga na klabu hiyo akiwa na imani kuwa Wenger atakabaki kama meneja kwa miaka kadhaa. (Evening Standard)
Steve Bould atachelewesha uamuzi ikiwa atabakia au la kama kaimu meneja wa Arsenal, anaposubiri kujua ni nani atakuwa meneja. (Telegraph)
West Ham walikutana na meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca saa chache baada ya mkataba wa meneja David Moyes kufika mwisho. (Mail)
David Moyes
West Ham watamfuta Moyes na watakuwa na majina matatu kwenye orodha yao. (Teamtalk)
Manchester City wanalenga kumsaini wing'a wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 25. (Star)
Manchester United wanakumbwa na upinzani kutoka kwa Paris St-Geraon kumsania kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred, 25. (Manchester Evening News)
Rafael Benitez
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anasema hana nia ya kurejea Napoli kwa kuwa yuko kwenye mazungumzo na Magpie kuhusu mkataba mpya. (Calcio Napoli 24 - in Italian)
Benitez amefanya mazungumzo na kipa wa Paris St-Germain Alphonse Areola, 29. (France Football - via Metro)
Real Madrid wako tayari kumwendea kipa Chelsea Thibaut Courtois, 26, wakati mbelgiji huyo akiingia miezi 12 ya mwiso ya mkataba wake.
Thibaut Courtois
Southampton wanataka kumsaini wing'a wa Celta Vigo Pione Sisto, 23. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark ana kipengee cha pauni milioni 36 cha kuondoka mapema kwenye mkataba wake.
Wing'a raia wa Morocco Sofiane Boufal, 24, amezungumzia nia yake ya kurejea ligi ya Ufaransa siku moja tu baada ya kukamilika kwa Premier League.(SFR Sport
Maoni