Watuhumiwa 11 wamekamatwa na jeshi lapolisi kwa wizi wa madini ya Tanzanite yenye gramu 1110 yenye thamani ya Tsh 5,551,234.92 yaliyoko ndani ya ukuta wenye kilo meter 24.5 uliojengwa kwenye mgodi wa 'Tanzanite one' ulioko Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Madini ya Tanzanite (Picha ya mtandaoni)
Kamanda wa polisi mkoani humo Agustino Senga akizungumza na waandishi wa habari amethibitisha kuibiwa kwa madini hayo na kusema kuwa watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani
Aidha Kamanda Senga amesema kwamba kwa sasa wanafanya tathmini ya kukagua migodi isiyotumika ili iweze kufungwa kutokana na kuwa migodi hiyo ndiyo inayotumika kuwa njia ya kuingilia kwenye migodi yenye madini.
Aidha Kamanda Senga amefafanua kuwa madini hayo yameibiwa na wachimbaji wadogo wadogo na wafanyakazi wa mgodi huo wa 'Tanzanite One' ambao wanauzoefu na mazingira ya maeneo hayo hivyo hutumia uzoefu wao kwa kutengeneza njia za panya maarufu kama mtobozano.
Madini hayo yaliyokamatwa kwasasa yamehifadhiwa katika ofisi ya madini Mererani
Maoni