Klabu ya soka ya Simba imesema inafanya usajili kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi, matakwa ya timu na ushiriki wa mashindano kwa msimu ujao na si pesa walizonazo, au kulipa kisasi kwa watani zao Yanga kama inavyosemwa sasa.
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaama na Msemaji wa timu hiyo Haji Sunday Manara, wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi za timu hiyo.
Manara amesema wachezaji waliokuwepo wamefanya kazi kubwa hivyo kwa hali ya msimu ujao wanahitaji watu wa ziada, wenye uzoefu kwaajili ya kuongeza nguvu zaidi.
āKwa wachezaji wa ndani ukimtoa Kaseja, Dida ndio golikipa aliyecheza mechi nyingi za kimataifa, hivyo Pascal Wawa amekuja kuziba pengo la Juuko aliye kwenda Afrika ya kusini kwa majaribio, Kagere tunaye kwasababu ya kuwasaidia Okwi na Bocco kila mtu anaujuwa uwezo wakeā , amesema Manara.
Mpaka sasa Simba imekamilisha Usajili wa wachezaji sita wapya wane wa ndani na wawili wa kimataifa, na kwa mujibu wa Msemaji wa Wekundu hao wa msimbazi ni kwambaa wataendelea kufanya hivyo kadili ya benchi la ufundi litakapo pendekeza
Maoni