Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.



Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.

Alijipatia kipato cha $275m (Ā£205m) katika mechi yake ya masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani.

Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo.

La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams kutoorodheshwa.

Wachezaji 100 bora walijipatia jumla ya $3.8bn, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 23 kutoka mwaka uliopita ,Forbes ilisema

Dereva wa magari ya F1 Lewis Hamilton ndio mwanamichezo Muingereza anayelipwa kipato cha juu cha $51m akiwa nambari 12.

Mayweather ambaye jina lake la utani ni Money-aliongeza kipato chake cha michezo kwa $10m

ā€œMechi kubwa kati yake na McGregor 2017 iliwasaidia Mayweather na McGregor kujipatia pato la jumla ya $400mā€ , alisema Kurt Badenhausen, Mhariri mkuu wa jarida wa Forbes Media.

ā€œLakini wachezaji wa mpira wa vikapu wametawala orodha ya wanamichezo 100 kufuatia kuongezwa kwa mishahara yao inayotokana na kandarasi ya maouyesho ya runinga ya $24bn

Aliongezea: ā€œOrodha ya Forbesā€™ ya wachezaji wanaopata mapato ya juu imejaa wanaume. lakini kumekuwa na mchezaji mmoja wa kike ambaye alifuzu baada ya orodha hiyo kuongezwa hadi majina 50 2010.

Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.

Floyd Mayweather ā€“ Ndondi ($285m)


Lionel Messi ā€“ Kandanda ($111m)


Cristiano Ronaldo -kandanda($108m)


Conor McGregor ā€“ Karate, judo na Ndondi ($99m)


Neymar ā€“ kandanda ($90m)


LeBron James ā€“ Vikapu ($85,5m)


Roger Federer ā€“ tenisi ($77.2m)


Stephen Curry ā€“ Vikapu ($76.9m)


Matt Ryan ā€“ Soka ya Marekani ($67.3m)


Matthew Stafford ā€“ Soka ya Marekani ($59.5m)


 

Marekani yatawala

Floyd Mayweather, Cristiano Ronaldo na Tiger Woods ā€“ wakiwa katika nambari 16 mwaka huu ndio wanamichezo watatu waliopo katika orodha ya wanamichezo tajiri zaidi ambao wamesalia katika orodha hiyo katika kipindi cha miaka 18 iliopita.

Mapato ya 2018 yalikuwa $22.9m, juu kutoka 1.5m mwaka uliopita kutokana na nyongeza ya mishahara miomgoni mwa wachezaji wa NBA.

Wanamichezo 11 kutoka michezo tofauti wameorodheshwa katika orodha hiyo na kutoka mataifa 22

Nyota wa ligi ya vikapu ya NBA wanaongoza katika orodha hiyo wakiwa wachezaji 40 miongoni mwa 100 tajiri.

Soka ya Marekani ndio mchezo wa pili uliowasilishwa sana ukiwa na wachezaji 18 , na kufuatiwa na mchezo wa baseball ukiwa na wachezaji 14 huku kandanda ikiwasilishwa na wachezaji 9 pekee.

Marekani ilitawala orodha hiyo ikiwa na wanariadha 66 huku Uingereza ikiwa na 5 wanaoongozwa na dereva wa F1 Lewis Hamilton katika nambari ya 12 na mapato ya $51m.

Mataifa ya Dominican na Uhispania yana wanariadha 3, hukiu Argentina, Brazil, Ufaransa, Japan na Venezuela wakiwa na wawili wawili.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...