Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli |
Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote.
*Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa.
Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1.
*Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro.
*Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo ajira nyingi za Waalimu na Madaktari zitazalishwa.
Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa amewasili nchini Tanzania Alhamis Juni 28, 2018 kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Hayo ndio matunda ya Tanzania kuimarika kwenye mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo, matunda ya ziara ya Rais wa Zimbabwe nchini Tanzania.
Pongezi kwa Rais Magufuli na Rais Mnangagwa kwa kujenga historia mpya.
Maoni